MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro, wameishukuru Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupitia mradi wa RISE kwa kuanza kukarabati barabara ya Mabogini–Kahe ambayo kwa miaka mingi ilikuwa katika hali mbaya na imekuwa chanzo cha adha kubwa kwa wakazi wa eneo hilo. Barabara hiyo yenye urefu … The post WANANCHI WA…
BRYSON MSHANA,MTWARA Utafiti unaoendelea kufanyika katika Kitalu cha Lindi–Mtwara, mkoani Mtwara umeonesha dalili za uwepo wa Gesi Asilia, hususani katika vijiji vya Mnyundo na Mpapura, mkoani Mtwara, ambapo visima vya maji vilibainika kuvujisha gesi asilia. Utafiti huo unajumuisha jumla ya vijiji 48 katika eneo la takriban kilomita za mraba 736 ambapo vijiji 40 vinatoka katika … The post DALILI…
BRYSON MSHANA, MTWARA Manispaa ya Mtwara-Mikindani mkoani Mtwara imesaini mkataba wa fedha zaidi ya shilingi bilioni 27 zinazolenga katika uboreshaji wa miundombinu ya mji kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Miji ya Tanzania (TACTIC) unaofadhiliwa na Serikali kuu kupitia mkopo wa Benki ya Dunia wenye thamani ya dola za Kimarekani Milioni 410 (Bila VAT). … The post ZAIDI YA BILIONI 27…
BRYSON MSHANA, MTWARA Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), imetangaza rasmi ratiba ya Korosho Marathon msimu wa nne, ambayo mwaka huu inatarajiwa kufanyika tarehe 29 Novemba 2025 na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi. Taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari leo tarehe 10 Octoba 2025 na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania … The post KOROSHO MARATHON MSIMU WA NNE…
BRYSON MSHANA, MTWARA Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameahidi kuwa serikali itaendelea kutoa ruzuku ya pembejeo bure kwa wakulima wa zao la korosho mkoani Mtwara, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kukuza kilimo na kuongeza kipato cha wakulim a vijijini. Dkt. Nchimbi alitoa ahadi hiyo … The post SERIKALI ITAENDELEA KUTOA RUZUKU YA PEMBEJEO…
BRYSON MSHANA, MTWARA Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) imeeleza kuwa maandalizi ya msimu mpya wa mauzo ya korosho ghafi wa mwaka 2025/2026 yanaendelea kwa vizuri, huku ikiahidi msimu wenye tija zaidi kwa wakulima na wadau wote wa tasnia hiyo. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliwasilishwa na Mkurugenzi wa Masoko na Udhibiti wa Ubora wa … The post CBT YAENDELEA NA MAANDALIZI YA MSIMU WA MAUZO YA KOROSHO…
BRYSON MSHANA, MTWARA Bandari ya Mtwara imefanikiwa kuongeza kiwango cha ufanisi katika kuhudumia shehena ya korosho baada ya kufanikisha usafirishaji wa jumla ya tani 370,896 katika msimu wa 2024/2025, ikilinganishwa na tani 253,616.94 za msimu wa 2023/2024. Taarifa hiyo imetolewa tarehe 29 septemba 2025, na Meneja wa Bandari ya Mtwara Ferdinand Nyathi, katika mkutano wa … The post BANDARI YA…
BRYSON MSHANA, LINDI Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kukamilika kwa mradi mkubwa wa uchakataji na usindikaji wa gesi asilia ya kimiminika (LNG) mkoani Lindi, mradi ambao umesimama kwa zaidi ya miaka 12. Akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika Lindi Mjini, Dkt. Samia alisema Serikali ipo … The post DKT. SAMIA AAHIDI NEEMA…
BRYSON MSHANA, MTWARA Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali Mkoa wa Mtwara, imefanya kikao cha kwanza cha Kamati ya ushauri wa kisheria, chenye lengo la kupeana majukumu na namna ya utekelezaji wake ikiwa ni pamoja na ushauri na uangalizi katika utekelezaji wa huduma za ushauri wa kisheria na Elimu ya Sheria kwa wananchi. Kikao hicho … The post OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MKOA WA MTWARA…
ABDUL LUKANGA, MTWARA Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Andrey Avetisyan, amefanya ziara rasmi ya kutembelea Bodi ya Korosho Tanzania mkoani Mtwara, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Urusi. Ziara hiyo imefanyika leo septemba 8/ ambapo ilimfikisha Balozi kwenye Kongani ya Viwanda inayoendelea kujengwa katika kijiji cha Maranje, … The post BALOZI WA…