Nenda kwa yaliyomo

Romania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
România
Romania
Bendera ya Romania Nembo ya Romania
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Wimbo wa taifa: Deşteaptă-te, române!
Lokeshen ya Romania
Mji mkuu Bukarest (Bucureşti)
44°25 N 26°06 E
Mji mkubwa nchini Bukarest
Lugha rasmi Kiromania
Serikali Jamhuri
Nicușor Daniel Dan
Ilie Bolojan
Uhuru
Ilitangazwa
ilitambiluwa
9 Mei 1877 (Kalenda ya Juliasi)2
13 Julai 18783
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
238,397 km² (ya 82)
2.97
Idadi ya watu
 - 2025 kadirio
 - 2021 sensa
 - Msongamano wa watu
 
19,043,151[1] (ya 65)
19,053,815[2]
83/km² (ya 132)
Fedha Leu (RON)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
EET (UTC+2)
EEST (UTC+3)
Intaneti TLD .ro
Kodi ya simu +40

-

1Lugha kama Kihungaria, Kijerumani, Kiromani, Kiukraine na Kiserbia hutumiwa kieneo kwenye ngazi kadhaa

2 Vita ya uhuru wa Romania.

3 Mkataba wa Berlin wa 1878.


Ramani ya Romania leo.
Falme tatu chini ya Mikaeli Shujaa (Mihai Viteazul) mwaka 1600 hivi.
Mlima Moldoveanu, mrefu kuliko yote ya Romania.
Milima ya Rodna, Wilaya ya Maramureș.
Delta ya mto Danube.

Romania (kwa Kiromania: România) ni nchi ya Ulaya ya kusini-mashariki.

Imepakana na Hungaria, Serbia, Ukraine, Moldova na Bulgaria.

Ina pwani kwenye Bahari Nyeusi ambako unaishia mto Danube.

Mji mkuu na mji mkubwa zaidi ni Bukarest.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Homo sapiens aliishi katika eneo hilo walau kuanzia miaka 40,000 iliyopita.

Kabla ya kutekwa na Warumi mwanzoni mwa karne ya 2, walikuwepo makabila ya Wathraki, hasa Wadacha na Wagete.

Chini ya Dola la Roma kwa miaka 165 kulikuwa na wahamiaji wengi walioingiza lugha ya Kilatini.

Baadaye nchi ilitekwa na makabila mengine mbalimbali.

Katika karne za kati kulikuwa na falme ndogo tatu: Wallachia, Moldavia na Transilvania, nazo ziliendelea kuwa na madaraka fulani hata chini ya Dola la Osmani hadi karne ya 18 au 19.

Romania ilianzishwa mwaka 1859 kwa kuunganisha Moldavia na Wallachia ikapewa jina hilo mwaka 1866, ikajikomboa kutoka dola la Osmani mwaka 1877.

Kutokana na vita vikuu vya kwanza, Transilvania, Bukovina na Besarabia viliungana na Ufalme wa Romania.

Katika vita vikuu vya pili, Romania iliunga mkono Ujerumani dhidi ya Muungano wa Kisovieti hadi mwaka 1944.

Wakomunisti waliteka nchi na baada ya vita kwisha, Romania ilipoteza maeneo mbalimbali na kulazimishwa kujiunga na Mapatano ya Warshawa kama jamhuri ya kisoshalisti.

Baada ya mapinduzi ya mwaka 1989, Romania ilielekea demokrasia na uchumi wa soko huria.

Baada ya kujiunga na Umoja wa Ulaya mwaka 2007, Romania imeanza kustawi na kwa sasa inaongoza pamoja na Malta zikiwa na ongezeko la 5% kwa mwaka.

Romania ina wakazi 19,043,151 katika eneo la km² 238.396. Idadi yao inazidi kupungua. Wengi ni Waromania asili (89.3%), Wahungaria asili ni 6%, Waromani ni 3.4%, wengineo ni 1.2%.

Lugha rasmi ya nchi nzima ni Kiromania ambayo ni lugha ya Kirumi kama Kiitalia, Kifaransa na Kihispania, lakini lugha nyingine kadhaa zinatambuliwa na sheria, kuanzia Kihungaria.

Wakazi wengi ni Wakristo (84.7%), hasa Waorthodoksi (73.6%), wakifuatwa na Waprotestanti (6.4%) na Wakatoliki (4.4%).

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "The usually resident population decreasing as of January 1st 2025 while the international migration balance remained positive in 2024" (PDF). www.insse.ro. INS. 14 Januari 2026. Iliwekwa mnamo 15 Januari 2026.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Populația după etnie la recensămintele din perioada 1930–2021". www.insse.ro (kwa Kiromania). INS. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Septemba 2023. Iliwekwa mnamo 4 Machi 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Romania kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.