Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Mahakama ya Katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwezi Julai, iliidhinisha sheria tata ya kufanyika kwa kura ya maoni, ili kuifanyia katiba mabadiliko baada ya kupitishwa na wabunge mwezi Juni. Hatua hii imewakera wapinzani wa rais Felix Tshisekedi, kutoka muungano wa C64 ambao wameitisha maandamano Septemba 15, baada ya kuchelewa kuanza kwa mazungumzo ya kitaifa. Tunachambua na mbunge…
Ni mwaka mmoja, kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya. Uchaguzi huo utafanyika tarehe 10 mwezi Agosti mwaka 2027. Wakenya watamchagua rais, Magavana, Maseneta, wabunge, wawakilishi wa kike na viongozi wa Wadi mbalimbali. Hata hivyo, joto la kampeni ya mapema, imeshaanza kushuhudiwa, hasa kwenye kinyanganyiro cha urais. Nini kimesababisha joto na kampeni za uchaguzi mkuu kuanza mapema nchini Kenya ?…
Nchini Tanzania, maneno maridhiano na Katiba mpya, yameendelea kutawala vinywa vya wanasiasa na wananchi wa taifa hilo baada ya uchaguzi mkuu uliokumbwa na vurugu wa Oktoba mwaka 2025. Hivi karibuni, rais Samia Suluhu Hassan alikutana nna viongozi wa vyama vya siasa na kutangaza mpango wa maridhiano na mchakato wa katiba mpya. Je, haya yanawezekana bila ushiriki wa chama cha upinzani CHADEMA,…
Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya 2027, nyota ya kisiasa ya Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna inaonekana kuanza kung'aa. Sifuna aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama cha ODM, sasa anaongoza vuguvugu linaloitwa Linda Mwananchi. Je, Sifuna ameanza kutembea kwenye viatu vya aliyekuwa kiongozi shupavu wa kisiasa, Marehemu Raila Odinga. Tunachambua.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi amekubali kuanzisha mazungumzo ya kitaifa kujadili mivutano ya kisiasa likiwemo suala la kuibadilisha katiba na changamoto za kiusalama mashariki mwa nchi hiyo. Tayari muungano wa maaskofu wa kanisa katoliki CENCO na ule wa makanisa ya Kiprotestanti, wameanza mashauriano na wadau mbalimbali kuhusu mchakato wa mazungumzo ya kitaifa. Je,…
Marekani na Iran zimeanza tena kushambuliana, na kuzua wasiwasi wa kuendelea kwa vita vilivyoanza mwezi Februari 2026. Mashambulizi haya yamelenga kudhibiti eneo la Bahari ya Hormuz, njia muhimu inayotumiwa na meli zinazosafirisha mafuta na gesi kuelekea katika maeneo mbalimbali ya dunia. Kwanini Marekani na Iran zimeanza tena kushamuliana na hii inamanisha nini ?
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, wiki hii amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa upinzani kutoka muungano wa C64 na viongozi wa Kanisa Katoliki na Kiprotestanti nchini DRC, wanaopinga mchakato wa marekebisho ya katiba unaoungwa mkono na rais Felix Tshisekedi. Je, rais Ndayishimiye, atafanikiwa kuleta maridhiano ?
Vita vimeendelea kushuhudiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kati ya wanajeshi na waasi wa M23/AFC wanaotuhumiwa kuungwa mkono na Rwanda licha ya Kigali na Kinshasa, kutia saini mkataba wa kusitisha vita mwaka mmoja uliopita. Kwanini vita vinaendelea licha ya kuwepo kwa mkataba huu ? Tunachambua.
Nchini Uganda, mwanasiasa wa upinzani na Meya wa zamani wa jiji la Kampala Erias Lukwago anakabiliwa na mashtaka ya uhaini. Alikamatwa nyumbani kwake na wanajeshi kwa agizo la Mkuu wa Majeshi Jenerali Muhoozi Kainerugaba na kuzuiwa kabla ya kufikishwa Mahakamani. Wiki hii, mwanasiasa mashuhuri na wakili wa Besigye Martha Karua kutoka nchini Kenya, alizuiwa kuingia nchini Uganda na kufukuzwa nchini…
Serikali ya Kenya, itaanza kuwalipa fidia watu karibu Elfu Mbili, walioathiriwa na visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwemo kuuawa, kubakwa, kutoweka na kujeruhiwa wakati wa maandamano ya kisiasa yaliyotokea nchini humo kati ya mwaka 2017 hadi 2025. Tume ya taifa ya haki za binadamu nchini Kenya, katika ripoti yake, inasema imewatambua waathiriwa wote wanaopaswa kupokea fidia hiyo, ambayo…