RSS Amplifier

Blog

Uhuru Publication

Ukweli Daima

uhurupublications.co.tzSource feed ↗15 posts

Live Last read · last published · next check

Written by

Latest posts

HATIMAYE

Na Waandishi Wetu HATIMAYE ile siku iliyosubiriwa kwa hamu na Watanzania, ni leo, ambayo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amezindua Bwawa la kihistoria la kuzalisha umeme la Julius Nyerere (JNHHP). JNHPP ni maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, aliyoyajenga na waasisi wenzake kuanzia mwaka 1976, hatimaye leo yametimia chini ya uongozi imara wa Rais […]

SAFARI KUTOKA STIEGLER’S GORGE HADI BWAWA LA JULIUS NYERERE

Na Ramadhani Semtawa ILIKUWA ndoto sasa ni halisi. Ndicho kinachoshuhudiwa na kusikika leo, kwa taifa kuzindua mradi mkubwa wa umeme wa Julius Nyerere, ambao awali ulijulikana Stiegler’s Gorge. Ni mradi wa kihistoria unaoendeleza msingi wa taifa kujitegemea, kwani unapunguza utegemezi wa ununuzi wa umeme kutoka nchi jirani na kulifanya taifa kuwa na zaida ya kuuza […]

TUNDU LISSU AKUTWA NA KESI YA KUJIBU

Na MWANDISHI WETU MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imemkuta Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ana kesi ya kujibu katika shauri la uhaini linalomkabili. Akisoma uamuzi huo Leo Agosti 21, 2026, Jaji Ndunguru, anayeongoza jopo la majaji linalosikiliza shauri hilo, amesema mahakama imejiridhisha kuwa upande wa […]

KUNENGE: JNHPP KUIMARISHA UPATIKANAJI UMEME NCHINI

Pwani Na Mwamvua Mwinyi MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, amesema uzinduzi wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), utakaofanyika kesho wilayani Rufiji mkoani hapa, ni atua kubwa ya kihistoria katika kuimarisha upatikanaji nishati ya uhakika nchini. Mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 za umeme unaotekelezwa kwa asilimia 60 katika […]

CCM YATAKA VIONGOZI WASIOYUMBA -WASIRA

Iramba NA MWANDISHI WETU MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amekemea viongozi wasiokuwa na msimamo ndani ya Chama, akisisitiza umuhimu wa kuzingatia haki kwa kutoegemea maslahi binafsi. Amesema CCM inahitaji viongozi wasioyumba katika masuala ya msingi, hivyo wanachama wanapaswa kuwapa uongozi watu wenye sifa za uadilifu. Wasira aliyasema hayo alipozungumza na […]

CCM INAHESHIMU UPINZANI–KIHONGOSI

Na REHEMA MAIGALA KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, amesema Chama kinaheshimu maoni ya wanasiasa na vyama vyote vya upinzani. MAWAZO MBADALA Pia, CCM imesisitiza iko tayari kuyafanyia kazi mawazo yenye msingi kutoka kwa vyama vya upinzani kwa maslahi mapana ya nchi. Kihongosi alisema hayo jijini Dar […]

PROF. KABUDI AWATAKA WANANCHI KUZINGATIA TAHADHARI ZA MAAFA

Na, Mwandishi wetu – Dar es Salaam WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu–Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Prof. Palamagamba Kabudi, amewataka wananchi kuzingatia tahadhari na maelekezo yanayotolewa na wataalamu na mamlaka husika ili kupunguza madhara yanayotokana na majanga na maafa. Prof. Kabudi ametoa wito huo Agosti 19, 2026, akizungumza katika maadhimisho ya Siku […]

WASIRA ATAKA WANA CCM WAKUTANE, WASIINGIE MKENGE KWA MANENO YA MITANDAONI

Na Mwandishi Wetu – Singida MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amewataka wanachama wa CCM kukutana mara kwa mara katika vikao rasmi vya chama ili kujadili masuala muhimu na kuepuka kupotoswa na taarifa zisizo na ukweli zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Akizungumza leo Agosti 19, 2026 Wilaya ya Ikungi mkoani Singida […]

TUTAENDELEA KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO YA UKIMWI – YONAZI

Na MWANDISHI MAALUMU, Shinyanga SERIKALI imesema itaendelea kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), kwa kuboresha vituo vya huduma, kuwezesha vikundi na kuimarisha ushirikiano na wadau, kuhakikisha Tanzania inatokomeza virusi hivyo ifikapo mwaka 2030.Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu na…

KETE NGUMU SIMBA, PAMBA JIJI

Na NASRA KITANA KIKOSI cha Simba leo kinashuka dimbani katika mchezo namba mbili, kumenyana na Pamba Jiji katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Simba itakuwa ugenini kupepetana na Pamba Jiji katika mechi itakayopigwa dimba la CCM Kirumba, Mwanza kuanzia majira ya saa 10:00 jioni. Timu hiyo yenye maskani yake Mtaa […]

MIAKA 50 YA UPUNGUFU WA MAFUTA YA KULA

Na JOE NAKAJUMO MOJA ya malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ni Tanzania kuwa mzalishaji mkuu wa chakula Afrika na kuwa miongoni mwa nchi 10 bora katika uzalishaji wa chakula. Kwa miaka kadhaa mfululizo, uzalishaji wa mazao ya chakula umekuwa ukiongezeka. Tani milioni 18 za mazao ya chakula zilizalishwa mwaka 2020/2021 na ziliongezeka hadi tani milioni […]

NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME KUTOKA BWAWA LA JULIUS NYERERE YA CHALINZE – DODOMA IMEKAMILIKA: MRAMBA

Na MWANDISHI WETU KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba, amesema Njia ya Kusafirisha Umeme ya Msongo wa Kilovolti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma imekamilika hatua itakayowezesha umeme unaozalishwa katika Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) kufika Dodoma kupitia Chalinze. Mramba ameyasema hayo leo, Agosti 18, 2026, akikagua hatua […]

SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA AFUA ZA UKIMWI NCHINI

Na Mwandishi Wetu, MWANZA SERIKALI imesema imedhamiria kuendelea kuimarisha afua za ukimwi nchini kwa kuboresha mazingira ya utekelezaji wa shughuli hizo, huku ikihimiza ushirikiano na wadau katika kuendeleza mapambano dhidi ya virusi hivyo. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dk. Jim Yonazi, alipotembelea na […]

FVS MWAROBAINI TLP KUPUNGUZA MAKOSA

ABDUL DUNIA Na NASRA KITANA WAKATI mechi za mzunguko wa kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara, msimu huu, zikimalizika mwisho mwa wiki, Teknolojia ya Usaidizi wa Video (FVS), imeelezwa inaweza kuwa tiba ya makosa ya waamuzi na kuleta usawa kwa timu katika kuamua matukio uwanjani. FVS ilianza kutumika katika mechi ya Ngao ya Jamii, iliyochezwa wiki […]

MKUCHIKA, LUBINGA, MNDOLWA WASIFU USHIRIKIANO CCM, SWAPO

Na SIMON NYALOBI BAADHI ya wanasiasa wakongwe nchini, wamesema ushirikiano baina ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vya ukombozi Kusini mwa Afrika, umezidi kuimarika. Waliyasema hayo zikiwa ni siku chache baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro, kufanya mazungumzo na Katibu wa Chama cha SWAPO cha Namibia, Sophia Shaningwa. Dk. Migiro na […]