# hali ngumu ya uchumi — RSS Amplifier

Recent posts from the 1 feeds in the RSS Amplifier directory that cover hali ngumu ya uchumi.

Page: <https://rssamplifier.com/topics/hali-ngumu-ya-uchumi>  
Feed: <https://rssamplifier.com/topics/hali-ngumu-ya-uchumi.md>

---

## [BI TAIFA &#8212; GLADYS KINUTHIA](https://taifaleo.nation.co.ke/bi-taifa/bi-taifa-gladys-kinuthia/)

_2026-08-27 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

Gladys Kinuthia ametimu miaka 25. Yeye ni mfanyabiashara kutoka Rongai. Uraibu wake ni kuimba,kutalii na kutangamana na marafiki wapya. PICHA|RICHARD MAOSI

## [Mbunge aandaa mbio za baiskeli kuboresha afya, kuhubiri amani](https://taifaleo.nation.co.ke/makala/mbunge-aandaa-mbio-za-baiskeli-kuboresha-afya-kuhubiri-amani/)

_2026-08-27 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

ZAIDI ya watu 500 walijitokeza eneo la Baharini, tarafa ya Mpeketoni, Lamu Magharibi kushuhudia mbio za baiskeli. Mashindano hayo yaliyodhaminiwa na ofisi ya Mbunge wa Kike wa kaunti ya Lamu, Bi Muthoni Monica Marubu yalidhamiria kuhubiri amani, umoja na utangamano msimu huu ambapo Uchaguzi Mkuu wa 2027 unaendelea kukaribia. Wakati wa mbio hizo, mashabiki waliojitokeza pamoja na walioshirikishwa…

## [Mke aliniambia hasikii mdundo wa ngoma, sasa naogopa hata kumkaribia!](https://taifaleo.nation.co.ke/makala/shangazi-akujibu/mke-aliniambia-hasikii-mdundo-wa-ngoma-sasa-naogopa-hata-kumkaribia/)

_2026-08-27 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

NILISHANGAA sana mke wangu kuniambia simridhishi kimapenzi. Badala ya kukasirika, nilihuzunika sana na nikaanza kujiona sitoshi mboga. Tangu siku hiyo nimekuwa nikiepuka hata kuanzisha ukaribu kwa sababu naogopa kukataliwa tena. Yeye sasa anasema hakukusudia kuniumiza, alitaka tu tuzungumze kuhusu kile ambacho kila mmoja anahitaji. Tatizo ni kwamba mimi nimeanza kujitenga kihisia. Nifanyeje?…

## [MAONI: Ushindani wa kisiasa usiwe wa kuvunja nchi wala kuibua uhasama](https://taifaleo.nation.co.ke/maoni/maoni-ushindani-wa-kisiasa-usiwe-wa-kuvunja-nchi-wala-kuibua-uhasama/)

_2026-08-27 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

MJADALA kuhusu amani na uwajibikaji wa viongozi unapaswa kupewa uzito unaostahili uchaguzi mkuu wa 2027 unapokaribia. Hivyo basi, Uzinduzi wa Mwongozo kuhusu Uchaguzi Usio na Vurugu wa 2027 uliotayarishwa na Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utengamano (NCIC) umejiri kwa wakati muafaka, ambapo dalili za kutovumiliana kisiasa, matamshi ya chuki na taarifa za kupotosha zinaanza kujitokeza. Historia ya…

## [Kesi kuhusu mauaji ya wapanga mikakati wa Ruto uchaguzi wa 2022 yasitishwa](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kitaifa/kesi-kuhusu-mauaji-ya-wapanga-mikakati-wa-ruto-uchaguzi-wa-2022-yasitishwa/)

_2026-08-27 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

MAHAKAMA Kuu jana ilizima kesi ya mauaji dhidi ya maafisa 15 wa usalama waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kuwateka na kuwaua raia wawili wa India na dereva wa teksi Mkenya kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2022. Jaji Francis Olel alikubali ombi la Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Renson Ingonga la kusitisha kesi hiyo hatua iliyohitimisha mashtaka yaliyokuwa yamesubiriwa kwa zaidi ya miaka miwili.…

## [DCI yachunguza picha iliyomsawiri Machele kama mhudumu harusini](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kaunti/dci-yachunguza-picha-iliyomsawiri-machele-kama-mhudumu-harusini/)

_2026-08-27 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

WAPELELEZI mjini Mombasa wanachunguza kisa cha picha ya Mbunge wa Mvita, Mohamed Machele, kubadilishwa na kuonyesha kana kwamba alikuwa mhudumu katika harusi ambako alikuwa mgeni mkuu, katika kile kinachodaiwa kuwa njama ya kumwaibisha. Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) imewasilisha ombi mahakamani ikitaka kupewa ruhusa ya kuchunguza simu ya mkononi inayohusishwa na aliyekuwa mshirika wa…

## [Muhoozi kuwania urais 2031 akisema babake, Rais Museveni, atamuunga mkono](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/kimataifa/muhoozi-kuwania-urais-2031-akisema-babake-rais-museveni-atamuunga-mkono/)

_2026-08-27 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

KAMPALA, Uganda: MKUU wa jeshi la Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mwana wa Rais Yoweri Museveni, ametangaza kuwa atawania urais katika uchaguzi wa mwaka 2031. Kainerugaba, mwenye umri wa miaka 52, kwa muda mrefu ametajwa kuwa mrithi anayetarajiwa wa baba yake mwenye umri wa miaka 81, ambaye ametawala Uganda kwa miongo minne. Mkuu huyo wa jeshi pia anafahamika kwa jumbe zake…

## [Gachagua sasa &#8216;ammaliza&#8217; Uhuru Mlimani na Nairobi](https://taifaleo.nation.co.ke/siasa/gachagua-sasa-ammaliza-uhuru-mlimani-na-nairobi/)

_2026-08-27 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

CHAMA cha DCP kinachoongozwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kinazidi kujitokeza kama tishio kubwa kwa Jubilee, chama cha aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta, huku kikivamia ngome zake za kisiasa za Mlima Kenya na Nairobi. Huku Uchaguzi Mkuu wa 2027 ukikaribia, Jubilee imepata pigo jingine, viongozi wake kadhaa waliochaguliwa wakitangaza kuhamia DCP. Mbunge wa Kamukunji Yusuf Hassan ndiye wa…

## [Ruto, Gachagua wang&#8217;ang&#8217;ania kura za Maasai huku Ole Lenku naye akikosana na ODM](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/ruto-gachagua-wangangania-kura-za-maasai-huku-ole-lenku-naye-akikosana-na-odm/)

_2026-08-27 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

VITA vya kisiasa vya kusaka kura za jamii ya Maa vinazidi kupamba moto kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027, huku Rais William Ruto na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua wakiongeza juhudi za kutafuta uungwaji mkono katika jamii ya wafugaji. Maa ina ushawishi mkubwa katika kaunti za Kajiado, Narok na Samburu, na pia ina idadi kubwa ya wakazi katika baadhi ya maeneo ya Laikipia. Takwimu za Tume Huru ya…

## [Sare baada ya sare: Wakuu wa usalama watetea mavazi mapya ya polisi](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kitaifa/sare-baada-ya-sare-wakuu-wa-usalama-watetea-mavazi-mapya-ya-polisi/)

_2026-08-27 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

MAAFISA wa polisi nchini wataanza kuvalia sare mpya kuanzia Ijumaa na kutelekeza ile ya rangi ya samawati iliyozinduliwa wakati wa utawala wa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta. Sare hizo mpya zitachukua nafasi ya sare za sasa zinazovaliwa na maafisa wa polisi wa kawaida, huku Polisi wa Utawala (APS) na Kitengo cha Kupambana na Ghasia (GSU) wakitarajiwa kuendelea kutumia sare zao za sasa. Inspekta…

## [Ship software peacefully (Sponsored)](https://crawlproof.com/a/SDQx6MuRshhi)

_2026-08-27 · **Sponsored**_

Deploy apps from your repo with auto-config, instant previews, scaling, and monitoring.

## [Mashirika ya usalama yalipewa Sh44.6 bilioni Julai, ongezeko kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kitaifa/mashirika-ya-usalama-yalipewa-sh44-6-bilioni-julai-ongezeko-kubwa-zaidi-kuwahi-kushuhudiwa/)

_2026-08-25 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

WIZARA ya Fedha ilitengea mashirika ya usalama jumla ya Sh44.6 bilioni mwezi Julai, hatua inayodhihirisha ufadhili mkubwa wa sekta hiyo katika mwaka wa mwisho wa serikali kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027. Kati ya fedha hizo, Wizara ya Ulinzi ilipokea Sh19.4 bilioni, huku Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) na Idara ya Usalama wa Ndani kila moja ikipokea Sh9.9 bilioni. Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi…

## [TAHARIRI: Gavana Ayacko awajibishwe kuhusiana na matamshi yake](https://taifaleo.nation.co.ke/tahariri/tahariri-gavana-ayacko-awajibishwe-kuhusiana-na-matamshi-yake/)

_2026-08-25 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

MATAMSHI ya Gavana wa Migori Ochilo Ayacko kuhusu ziara inayopangwa ya Gavana wa Siaya James Orengo na viongozi wengine wa vuguvugu la Linda Mwananchi yanatia wasiwasi na yanastahili kulaaniwa vikali. Kauli hii imetolewa wiki moja tu baada ya ghasia za kisiasa katika Kaunti ya Homa Bay kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhiwa kwa wengine kadhaa. Kenya inahitaji viongozi wa kisiasa kupunguza…

## [Serikali Zambia yazuia upinzani kuwasilisha kesi kupinga matokeo; yafunga mahakama kuu](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/kimataifa/serikali-zambia-yazuia-upinzani-kuwasilisha-kesi-kupinga-matokeo-yafunga-mahakama-kuu/)

_2026-08-25 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

LUSAKA, Zambia: SERIKALI ya Zambia ilifunga mahakama kuu za nchi hiyo Jumatatu, ili kuwazuia watu kuingia katika majengo hayo siku ya mwisho ambayo upinzani ungeweza kuwasilisha kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wenye utata uliofanyika mwezi huu. Barua kutoka kwa msimamizi mkuu wa idara ya mahakama, ambao Reuters iliona, ilisema kwamba, “kwa sababu za kiusalama, wafanyakazi wote wanashauriwa…

## [Nchimbi agusia Samia katika sababu za kujiuzulu: &#8216;Nimeona Rais anatamani mabadiliko&#8217;](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/kimataifa/nchimbi-agusia-samia-katika-sababu-za-kujiuzulu-nimeona-rais-anatamani-mabadiliko/)

_2026-08-25 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

DAR ES SALAAM, Tanzania: MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Dkt Emmanuel John Nchimbi, Jumanne, Agosti 25, 2026 alitangaza uamuzi wake wa kujiuzulu wadhifa wake na kustaafu kabisa katika utumishi wa umma na siasa kuanzia Septemba 4, 2026. Katika taarifa rasmi kwa umma iliyotolewa na Afisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma, Dkt Nchimbi alisema tayari amemkabidhi Rais Samia Suluhu Hassan barua rasmi ya…

## [Gavana asihi wakazi wa Taita Taveta wasiunge Gachagua](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kaunti/gavana-asihi-wakazi-wa-taita-taveta-wasiunge-gachagua/)

_2026-08-25 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

VIONGOZI wa Taita-Taveta wakiongozwa na Gavana Andrew Mwadime wamewaonya wakazi wa Pwani dhidi ya kuunga mkono siasa za upinzani zinazoongozwa na kinara wa chama cha DCP, Bw Rigathi Gachagua. Bw Mwadime alisema Bw Gachagua hafai kupata uungwaji mkono kutoka eneo la Pwani kwa sababu hakufanya lolote la maana kwa eneo hilo alipokuwa Naibu wa Rais baada ya uchaguzi mkuu wa 2022. Alisema Bw Gachagua…

## [Mtoto, 4, alivyounganishwa na mamake aliyefurushwa Saudi Arabia](https://taifaleo.nation.co.ke/makala/mtoto-4-alivyounganishwa-na-mamake-aliyefurushwa-saudi-arabia/)

_2026-08-25 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

MTOTO mwenye umri wa miaka minne, Precious Wambui, ameunganishwa tena na mamake Kenya baada ya kuishi Saudi Arabia kwa miaka mitatu kufuatia kufurushwa kwa mamake, Penina Wanjiru, 2025. Precious aliwasili Nairobi Jumatatu na kukutanishwa na mamake katika afisi za Idara ya Serikali ya Masuala ya Wakenya Wanaoishi Nje ya Nchi. Bi Wanjiru alisema anafurahi kurejeshewa mwanawe baada ya kipindi kigumu…

## [Ruto azungumzia siku za mwisho na Raila akisema alimwambia alishatoka hospitali](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kitaifa/ruto-azungumzia-siku-za-mwisho-na-raila-akisema-alimwambia-alishatoka-hospitali/)

_2026-08-25 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

RAIS William Ruto ameeleza jinsi alivyopokea taarifa ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, mauti ambayo yalizua wingu la huzuni na kutumbukiza taifa kwenye wimbi la maombolezo. Kwenye mahojiano na Taifa Leo , Rais Ruto alisema alikuwa akielekea afisini mwake mwendo wa saa 12:30 asubuhi Oktoba 15, 2025, simu yake ilipokereza. Simu hiyo ilipigwa na Seneta wa Siaya Dkt Oburu Oginga, kakake…

## [Kauli ya Wetang&#8217;ula kwamba ajira za TSC hugawiwa wabunge Ikulu yachemsha vyama](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kitaifa/kauli-ya-wetangula-kwamba-ajira-za-tsc-hugawiwa-wabunge-ikulu-yachemsha-vyama/)

_2026-08-25 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

VYAMA vya walimu vimekasirishwa na matamshi ya Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula kwamba baadhi ya wabunge hupewa barua za ajira za Tume ya Kuwaajiri Walimu (TSC) katika Ikulu. Chama cha Walimu Nchini (KNUT), Muungano wa Walimu wa Shule za Upili na Vyuo vya Anuwai (KUPPET) na Muungano wa Walimu wanaofundisha maeneo kame (KETHAWA), wote wamesema kauli hiyo imeibua upya madai ya mapendeleo…

## [Atwoli: Wakati wetu tukiwa Azimio kumfikia Uhuru ilikuwa ngumu, wala hakufanya mengi](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kitaifa/atwoli-wakati-wetu-tukiwa-azimio-kumfikia-uhuru-ilikuwa-ngumu-wala-hakufanya-mengi/)

_2026-08-25 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

KATIBU Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (COTU), Francis Atwoli, sasa anadai ilikuwa vigumu kumfikia Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, akidai kwamba mara nyingi alisita kushirikiana na mawaziri na viongozi wa kisiasa kuhusu masuala muhimu ya kitaifa. Akizungumza Khwisero, Kaunti ya Kakamega, jana Bw Atwoli alisema Bw Kenyatta alikuwa mgumu kufikiwa ikilinganishwa na marais wengine aliowahi…

## [Ayacko: Hatutaki viongozi wa Linda Mwananchi Migori](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kitaifa/ayacko-hatutaki-viongozi-wa-linda-mwananchi-migori/)

_2026-08-25 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

GAVANA wa Migori Ochilo Ayacko amewaonya viongozi wa kundi la Linda Mwananchi dhidi ya kuzuru kaunti hiyo, akisema ziara yao iliyopangwa inaweza kuongeza joto la kisiasa na kusababisha ghasia kama zile zilizoshuhudiwa hivi karibuni katika Kaunti ya Homa Bay. Onyo hilo linatolewa wiki moja baada ya mapigano kati ya wafuasi wa ODM na kundi la Linda Mwananchi huko Homa Bay kusababisha vifo vya watu…

## [Reach prospects with real signals (Sponsored)](https://crawlproof.com/a/Okw9dS8mUi5K)

_2026-08-25 · **Sponsored**_

Find prospects talking about your problem and get context-backed moments to engage

## [Ruto atua ngome ya Kalonzo na minofu uchaguzi ukikaribia](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/ruto-atua-ngome-ya-kalonzo-na-minofu-uchaguzi-ukikaribia/)

_2026-08-23 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

RAIS William Ruto amewataka viongozi wa upinzani kutafuta hoja bora za kupinga ajenda yake ya maendeleo badala ya kuwagawanya Wakenya kwa misingi ya ukabila. Rais alisema hayo jana alipofanya ziara katika Kaunti ya Machakos, ngome ya kisiasa ya kiongozi wa Wiper Patriotic Front Kalonzo Musyoka, huku akijaribu kuvutia wakazi wa Ukambani kuelekea uchaguzi wa 2027. Rais pia alishutumu upinzani kwa…

## [Kindiki asema atazima kabisa nyota ya Gachagua Mlimani](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/kindiki-asema-atazima-kabisa-nyota-ya-gachagua-mlimani/)

_2026-08-23 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

NAIBU Rais Kithure Kindiki amesema yuko tayari kumkabili mtangulizi wake Rigathi Gachagua katika vita vinavyozidi kupamba moto vya kudhibiti siasa za Mlima Kenya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Prof Kindiki na Bw Gachagua wanadai kuwa wana ushawishi mkubwa katika eneo hilo lenye wapigakura wengi, huku kila mmoja akijigamba kuwa ana uwezo wa kumbwaga mwenzake katika uchaguzi ujao. Bw Gachagua…

## [Ndindi Nyoro akoroga hesabu za Gachagua Mlimani](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/ndindi-nyoro-akoroga-hesabu-za-gachagua-mlimani/)

_2026-08-23 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

KIONGOZI wa chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP), Rigathi Gachagua anakabiliwa na changamoto mpya katika juhudi zake za kudhibiti siasa za eneo la Mlima Kenya, mwezi mmoja tu baada ya ushindi mkubwa wa chama chake katika uchaguzi mdogo wa Ol Kalou. Katika uchaguzi huo wa Julai 17, mgombeaji wa DCP, Kamau Ngotho alipata kura 35,440, sawa na asilimia 85 ya kura zote, dhidi ya mgombeaji…

## [Tiketi ya Sifuna–Kalonzo yaendelea kupigiwa debe](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/tiketi-ya-sifuna-kalonzo-yaendelea-kupigiwa-debe/)

_2026-08-23 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

UCHAGUZI Mkuu wa 2027 unapokaribia, upinzani unaanza kuashiria mwelekeo wa kuungana na vuguvugu la Linda Mwananchi, huku mjadala kuhusu nani atabeba bendera ya urais ukizidi kupamba moto. Katika ishara ya mwelekeo huo, Seneta wa Kakamega Boni Khalwale ameibua uwezekano wa tiketi ya Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na Kalonzo Musyoka, akidai kuwa muungano huo unaweza kupatia upinzani nafasi nzuri ya…

## [Ruto adai Uhuru amekataa handisheki licha ya juhudi zake za kutaka wapatanishwe](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/ruto-adai-uhuru-amekataa-handisheki-licha-ya-juhudi-zake-za-kutaka-wapatanishwe/)

_2026-08-23 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

HAKUNA siri kwamba uhusiano kati ya Rais William Ruto na mtangulizi wake Uhuru Kenyatta umeharibika. Lakini kiwango cha uhasama kati ya viongozi hao wawili, ambao wakati mmoja walionekana kuwa washirika wasioweza kutenganishwa, unaonekana katika juhudi za Rais Ruto za miaka minne zilizolenga kurejesha uhusiano wao. Katika mahojiano ya kipekee na Taifa Jumapili katika Ikulu ya Nairobi Ijumaa,…

## [Mke wa Besigye aomba kesi inayomwandama mumewe iahirishwe hadi apate nafuu](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/kimataifa/mke-wa-besigye-aomba-kesi-inayomwandama-mumewe-iahirishwe-hadi-apate-nafuu/)

_2026-08-22 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

MKE wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, Winnie Byanyima, amelaani kuendelea kwa kesi ya mumewe huku mwanasiasa huyo akiwa amelazwa kutokana na hali yake mbaya ya afya. Besigye, 70, anakabiliwa na mashtaka ya uhaini yanayohusiana na madai ya kupanga njama ya kumpindua Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986. Byanyima, ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS,…

## [Siasa: IEBC yapiga breki kampeni katika maeneo ya ibada, mazishini](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/siasa-iebc-yapiga-breki-kampeni-katika-maeneo-ya-ibada-mazishini/)

_2026-08-22 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imewapa wanasiasa na wanaowania nyadhifa mbalimbali waliochapisha mabango ya kampeni yenye nembo ya tume hiyo siku tano kuyaondoa mara moja, ikiongeza juhudi za kukabiliana na kampeni za mapema kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Agosti 10, 2027. Katika taarifa kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo, IEBC ilisema matumizi ya nembo yake \[…\]

## [Azma ya Omar kuwania ugavana Mombasa yaleta mgawanyiko kati ya UDA na ODM Pwani](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/azma-ya-omar-kuwania-ugavana-mombasa-yaleta-mgawanyiko-kati-ya-uda-na-odm-pwani/)

_2026-08-22 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

TANGAZO la Katibu Mkuu wa UDA, Hassan Omar kuwania ugavana Mombasa mwaka 2027 limezua mgawanyiko katika ushirikiano unaoibuka kati ya UDA na ODM, huku juhudi za kugawana maeneo ya kisiasa Pwani zikikabiliwa na changamoto. Bw Omar ametangaza kuwa ataendelea na azma yake ya kuwania kiti hicho, hatua inayotishia mpango wa vyama hivyo kuepuka kushindana moja kwa moja katika baadhi ya kaunti. Kwa zaidi…

## [Gachagua ataka FBI ichunguze ajali ya ndege iliyomwangamiza Ng’eno](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/gachagua-ataka-fbi-ichunguze-ajali-ya-ndege-iliyomwangamiza-ngeno/)

_2026-08-22 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

ALIYEKUWA Naibu Rais, Rigathi Gachagua ametaka maafisa kutoka Scotland Yard ya Uingereza na Shirika la Upelelezi la Amerika (FBI) waalikwe nchini kuchunguza ajali ya helikopta iliyomuua aliyekuwa Mbunge wa Emurua Dikirr Johana Ng’eno na watu wengine watano. Bw Gachagua alisema Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kenya (KCAA) haziwezi \[…\]

## [Walinzi wa Nassir wadaiwa kufyatulia vijana risasi](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/walinzi-wa-nassir-wadaiwa-kufyatulia-vijana-risasi/)

_2026-08-22 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

WATU watatu walijeruhiwa baada ya walinzi wanaodaiwa kuwa wa Gavana wa Mombasa, Abdulswamad Nassir kufyatua risasi katika hafla ya umma katika Uwanja wa Bomu, Changamwe, Mombasa, Ijumaa alasiri. Tukio hilo lilitokea wakati wa mkutano wa kuhamasisha wananchi kuhusu mpango wa Biashara Mtaani, unaoendeshwa kupitia Hazina ya Mzunguko ya Kaunti ya Mombasa kwa wakazi wa Changamwe na Jomvu. Kamanda wa…

## [Build with the cheapest GPUs (Sponsored)](https://crawlproof.com/a/ZsHIs1Pwc2iP)

_2026-08-22 · **Sponsored**_

Deployed a live API in minutes; one user spent under $10.

## [Ajabu mapanga sasa yakigeuzwa silaha kali ya wahuni](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kitaifa/ajabu-mapanga-sasa-yakigeuzwa-silaha-kali-ya-wahuni/)

_2026-08-22 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

MAPANGA yanabadilishwa kutoka zana ya kawaida ya shambani kuwa silaha ya kutisha na kuwashambulia watu, huku ripoti ya kijasusi ikifichua kuwa angalau mapanga 500 yalisambazwa kwa vijana waliozua vurugu wakati wa ziara ya Linda Mwananchi, Homa Bay. Huku joto la kisiasa likipanda kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027, vijana wanaobeba mapanga katika mikutano ya hadhara na makabiliano ya kisiasa wamekuwa…

## [Athari za dawa za kufisha ganzi wakati wa kujifungua kwa upasuaji](https://taifaleo.nation.co.ke/makala/afya-na-jamii/athari-za-dawa-za-kufisha-ganzi-wakati-wa-kujifungua-kwa-upasuaji/)

_2026-08-21 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

KWA Atieno, kumbukumbu ya siku aliyomkaribisha kifungua mimba wake duniani haikujumuisha tu furaha ya kumwona mwanawe, bali pia hofu aliyokuwa nayo kabla ya kujifungua kwa upasuaji (Caesarean Section). Alipofahamishwa kuwa angelazimika kujifungua kwa upasuaji, jambo lililomtisha zaidi halikuwa upasuaji wenyewe bali sindano ya kufisha ganzi inayodungwa kwenye uti wa mgongo. Alikuwa amesikia kutoka…

## [Wakazi wataka maisha bora baada ya ujangili kuzimwa mpakani](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kaunti/wakazi-wataka-maisha-bora-baada-ya-ujangili-kuzimwa-mpakani/)

_2026-08-21 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

KWA zaidi ya miongo mitatu, wakazi wa Lorogon, mpakani mwa Turkana na West Pokot, wameishi kwa hofu ya majangili wenye silaha. Lakini sasa bunduki zimetulia kwa kiasi kikubwa kufuatia operesheni ya serikali ya kuwapokonya silaha wahalifu hao, na wakazi wanataka amani hiyo iwaletee ajira, maji, umeme na maisha bora. Lorogon iko kati ya Mto Turkwel na vilima vyenye mabonde magumu kufikika, ambayo…

## [Maafisa waagizwa kupigia debe mafanikio ya serikali kuelekea 2027](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kitaifa/maafisa-waagizwa-kupigia-debe-mafanikio-ya-serikali-kuelekea-2027/)

_2026-08-21 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

SERIKALI ya Rais William Ruto imeanza kuimarisha kampeni ya mawasiliano kwa umma kuhusu sera, miradi na mafanikio yake huku uchaguzi mkuu wa 2027 ukikaribia. Hatua hiyo inafuatia barua ya Mkuu wa Utumishi wa Umma na Wafanyakazi wa Ikulu, Felix Koskei, kwa mawaziri, makatibu, msemaji wa serikali na wakuu wa mashirika ya serikali. Katika barua iliyoandikwa Agosti 17, 2026, Bw Koskei aliwaagiza…

## [Faili ya uchunguzi wa mlinzi wa Katibu Fikirini Jacobs yafungwa](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kitaifa/faili-ya-uchunguzi-wa-mlinzi-wa-katibu-fikirini-jacobs-yafungwa/)

_2026-08-21 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

MAHAKAMA ya Makadara imefunga faili ya uchunguzi dhidi ya mlinzi wa Katibu wa Masuala ya Vijana, Fikirini Jacobs kuhusu kupigwa risasi na kuuawa kwa kiongozi wa vijana mtaani Kariokor, Cecil Ouma, huku ikisubiri uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP). Mahakama ilisema faili hilo haiwezi kuendelea kuwa wazi kusubiri wachunguzi kukamilisha mchakato wa kuwasilisha ripoti ya uchunguzi wa…

## [Afisa wa polisi aliyeuawa Homa Bay alikuwa akisubiri kupandishwa cheo](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kitaifa/afisa-wa-polisi-aliyeuawa-homa-bay-alikuwa-akisubiri-kupandishwa-cheo/)

_2026-08-21 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

KONSTABO Jim Richardson Onkundi, aliyefariki baada ya kupigwa na jiwe wakati wa mkutano wa Linda Mwananchi Homa Bay, alikuwa akisubiri kupandishwa cheo kuwa koplo. Onkundi, 36, alikuwa akiendesha gari la polisi lililokuwa limewabeba maafisa watano kutoka Kituo cha Polisi cha Chemelil, Muhoroni, Kaunti ya Kisumu. Alikuwa amemaliza mafunzo ya kupandishwa cheo katika Chuo cha Polisi Kiganjo na…

## [Mapanga 500 na silaha zingine zilisambaziwa wahuni Homa Bay, polisi wafichua](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kitaifa/mapanga-500-na-silaha-zingine-zilisambaziwa-wahuni-homa-bay-polisi-wafichua/)

_2026-08-21 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

TAKRIBAN vijana 500 walilipwa kuziba barabara kuwazuia wafuasi wa Linda Mwananchi kuingia Homa Bay wakati wa mkutano wao Jumapili iliyopita, huku polisi wakifichua kuwa mapanga 500 na silaha nyingine zilisambazwa kabla ya ghasia hizo. Ripoti ya kijasusi iliyotayarishwa baada ya polisi kunasa silaha hizo imeibua wasiwasi kuhusu kiwango cha maandalizi yaliyofanyika kabla ya mkutano wa Agosti 16.…

## [Gachagua aapa kutembea Emurua Dikirr licha ya vitisho](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kitaifa/gachagua-aapa-kutembea-emurua-dikirr-licha-ya-vitisho/)

_2026-08-21 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

NAIBU Rais Rigathi Gachagua ameapa kutembelea Emurua Dikirr, Narok, leo Ijumaa licha ya vitisho kutoka kwa viongozi wa eneo hilo. Chama chake cha Democracy for Citizens Party (DCP) kimesema Bw Gachagua atatumia ziara hiyo kuwashukuru wakazi waliounga mkono chama hicho katika uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika hivi majuzi. Pia, anatarajiwa kuzungumzia masuala ya ardhi na kile anachodai ni…

## [Bunge lapitisha sheria kutatua msongamano shule za kitaifa](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/bunge-lapitisha-sheria-kutatua-msongamano-shule-za-kitaifa/)

_2026-08-20 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

SHULE za jamii, zilizo katika kundi la C4, huenda zikanufaika pakubwa na mpango mpya wa usajili wa wanafunzi wa Gredi 10 unaopendekezwa kuanza Januari 2027. Wabunge wamepitisha kwa kauli moja hoja inayotaka Wizara ya Elimu, kwa ushirikiano na taasisi nyingine, kuweka idadi ya mikondo ambayo kila kundi la shule linaweza kuwa nayo. Chini ya pendekezo hilo, shule za kitaifa zilizo kundi la C1…

## [MAONI: Tuzoee kama nchi kukubali maoni na mitazamo kinzani](https://taifaleo.nation.co.ke/maoni/maoni-tuzoee-kama-nchi-kukubali-maoni-na-mitazamo-kinzani/)

_2026-08-20 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

KADRI uchaguzi mkuu unavyojongea ndivyo tabia ya kufadhaisha isiyoruhusu mtazamo na msimamo tofauti inavyozidi kujitokeza. Katika taifa linalojivunia demokrasia na utawala wa kikatiba, ungetarajia sote tunafahamu kila mwananchi, awe raia wa kawaida au kiongozi, amehakikishiwa kufurahia haki na uhuru kikatiba mradi hatoingilia uhuru na haki za mwananchi mwenzake. Ni kinaya kuwaona watu mashuhuri…

## [Mundubile kupinga ushindi wa Hichilema mahakamani](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/kimataifa/mundubile-kupinga-ushindi-wa-hichilema/)

_2026-08-20 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

LUSAKA, Zambia: KIONGOZI wa upinzani Zambia, Brian Mundubile, Alhamisi alisema atapinga matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 13 kortini, akidai kuwa kulikuwa na udanganyifu na ukiukaji mkubwa wa haki. Mundubile alisema Jumatano jioni kuwa kampeni yake imekusanya ushahidi wa kasoro katika mchakato wa uchaguzi, kuhesabiwa kwa kura, kutumwa kwa matokeo na kutangazwa kwake. “Kampeni yetu…

## [Kenya kuagiza magunia milioni 25 ya mahindi ukame ukipunguza uzalishaji](https://taifaleo.nation.co.ke/makala/kenya-kuagiza-magunia-milioni-25-ya-mahindi-ukame-ukipunguza-uzalishaji/)

_2026-08-20 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

KENYA inapanga kuagiza magunia milioni 25 ya mahindi ili kuziba pengo la nafaka hiyo lililosababishwa na ukame unaoendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini yanayotegemewa kwa uzalishaji wake. Kwenye mahojiano ya kipekee na Taifa Leo Dijitali, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Mutahi Kagwe, alisema uagizaji huo utafanywa na sekta binafsi. “Ni sekta binafsi itakayonunua mahindi.…

## [Mkuu wa runinga ya Telemundo, mkuu wa Ujasusi Ecuador miongoni mwa 7 waliofariki ajali ya helikopta](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/mkuu-wa-runinga-ya-telemundo-mkuu-wa-ujasusi-ecuador-miongoni-mwa-7-waliofia-kwa-helikopta/)

_2026-08-20 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

WATU saba walioangamia katika ajali ya helikopta Mlima Ololokwe, Samburu walijumuisha Mkenya, Waamerika watano na raia wa Ecuador. Waliofariki wanajumuisha rubani Mkenya na mkurugenzi wa kampuni ya African Heli Adventures Josh Outram, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Ujasusi cha Ecuador Michele Sensi-Contugi na mkewe Stephany Hollihan Yeaza. \[caption id="attachment\_191376" align="alignnone"…

## [Binti aonya mamake akome kuchekacheka na mume wake](https://taifaleo.nation.co.ke/dondoo/binti-aonya-mamake-akome-kuchekacheka-na-mume-wake/)

_2026-08-20 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

KATIKA tukio lisilo la kawaida,msupa mmoja wa hapa alimpigia mamake simu na kumuonya vikali akome kucheka cheka na mumewe kila mara. Mwanadada huyo alishuku kwamba wawili hao walikuwa kwenye uhusiano wa kisiri baada ya jamaa kutoa usemi kwamba mama-mkwe alikuwa amedumisha urembo wake. Matamshi hayo yalimshtua mwanadada huyo aliyehisi kwamba mumewe alikuwa na lengo la kunyemelea mama mkwe. Demu…

## [Wanafunzi wengi wa Gredi 9 hawawezi kusoma ipasavyo -Ripoti](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kitaifa/wanafunzi-wengi-wa-gredi-9-hawawezi-kusoma-ipasavyo-ripoti/)

_2026-08-20 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

TAKRIBAN thuluthi moja ya wanafunzi wanaojiunga na Sekondari Pevu kutoka Sekondari Msingi hawana ujuzi muhimu wa kusoma, kuandika na kuhesabu, ripoti mpya imefichua. Ripoti hiyo iliyotolewa na Usawa Agenda, shirika linalofanya utafiti kuhusu elimu ya msingi, pia imeonyesha kuwa wanafunzi katika shule za umma za maeneo ya mashambani ndio walioathirika zaidi. Utafiti huo uliofanywa katika kaunti…

## [Benki ya Equity yaripoti kuvuna faida kemkem ikielezea kuimarika sekta ya mikopo na akiba](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/benki-ya-equity-yaripoti-kuvuna-faida-kemkem-ikielezea-kuimarika-kwa-biashara-zake/)

_2026-08-20 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

EQUITY Group Holdings imeripoti ongezeko la asilimia 32 la faida baada ya ushuru katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, ikiashiria kuimarika kwa biashara yake nchini Kenya na katika matawi yake ya kikanda. Benki hiyo ilisema jana faida baada ya ushuru ilipanda hadi Sh45.5 bilioni kutoka Sh34.6 bilioni katika kipindi kama hicho mwaka jana. Faida kabla ya ushuru iliongezeka kwa asilimia 39 hadi…

## [Mwanamume kulipa mpenziwe wa zamani Sh2.5m baada picha za siri kusambaa mitandaoni](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/mwanamume-kulipa-mpenziwe-wa-zamani-sh2-5m-baada-picha-za-siri-kusambaa-mitandaoni/)

_2026-08-20 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

MAHAKAMA Kuu imeamuru mwanamume mmoja kumlipa Sh2.5 milioni mwanamke aliyeolewa baada ya picha zake za uchi kusambaa mtandaoni, ikisema mtu anayemiliki picha za siri za mwingine ana wajibu wa kuzilinda. Mahakama ilisema kutozuia picha hizo kusambazwa bila idhini kunaweza kumfanya mhusika kuwajibika, hata kama mwathiriwa hawezi kuonyesha moja kwa moja akaunti iliyozichapisha. Mwanamume huyo, GH,…

## [Wataalamu waeleza kwa nini kuna baridi kali Nairobi mwezi huu wa Agosti](https://taifaleo.nation.co.ke/habari/habari-za-kitaifa/wataalamu-waeleza-kwa-nini-kuna-baridi-kali-nairobi-mwezi-huu-wa-agosti/)

_2026-08-20 · Fatuma Bariki · Taifa Leo_

KWA Wakenya wengi, Agosti umekuwa mwezi wa kuvaa nguo nzito, kujifunika blanketi na baridi kali isiyo ya kawaida asubuhi. Nairobi na maeneo ya nyanda za juu katikati mwa nchi yamekuwa yakishuhudia hali hiyo hadi mchana, jambo linalowafanya wengi kujiuliza ni kwa nini ilhali msimu wa kiangazi unakaribia kufika mwisho. Lakini wataalamu wa masuala ya hali ya hewa wanasema baridi ya Agosti si jambo…

