RSS Amplifier

Blog

Taifa Leo

taifaleo.nation.co.keSource feed ↗28 posts

Overdue Last read · last published · next check
Last read 3 days ago, longer than this feed's 1 hour schedule.

Written by

Latest posts

Ruto atua ngome ya Kalonzo na minofu uchaguzi ukikaribia

RAIS William Ruto amewataka viongozi wa upinzani kutafuta hoja bora za kupinga ajenda yake ya maendeleo badala ya kuwagawanya Wakenya kwa misingi ya ukabila. Rais alisema hayo jana alipofanya ziara katika Kaunti ya Machakos, ngome ya kisiasa ya kiongozi wa Wiper Patriotic Front Kalonzo Musyoka, huku akijaribu kuvutia wakazi wa Ukambani kuelekea uchaguzi wa 2027. Rais pia alishutumu upinzani kwa…

Kindiki asema atazima kabisa nyota ya Gachagua Mlimani

NAIBU Rais Kithure Kindiki amesema yuko tayari kumkabili mtangulizi wake Rigathi Gachagua katika vita vinavyozidi kupamba moto vya kudhibiti siasa za Mlima Kenya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Prof Kindiki na Bw Gachagua wanadai kuwa wana ushawishi mkubwa katika eneo hilo lenye wapigakura wengi, huku kila mmoja akijigamba kuwa ana uwezo wa kumbwaga mwenzake katika uchaguzi ujao. Bw Gachagua…

Ndindi Nyoro akoroga hesabu za Gachagua Mlimani

KIONGOZI wa chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP), Rigathi Gachagua anakabiliwa na changamoto mpya katika juhudi zake za kudhibiti siasa za eneo la Mlima Kenya, mwezi mmoja tu baada ya ushindi mkubwa wa chama chake katika uchaguzi mdogo wa Ol Kalou. Katika uchaguzi huo wa Julai 17, mgombeaji wa DCP, Kamau Ngotho alipata kura 35,440, sawa na asilimia 85 ya kura zote, dhidi ya mgombeaji…

Tiketi ya Sifuna–Kalonzo yaendelea kupigiwa debe

UCHAGUZI Mkuu wa 2027 unapokaribia, upinzani unaanza kuashiria mwelekeo wa kuungana na vuguvugu la Linda Mwananchi, huku mjadala kuhusu nani atabeba bendera ya urais ukizidi kupamba moto. Katika ishara ya mwelekeo huo, Seneta wa Kakamega Boni Khalwale ameibua uwezekano wa tiketi ya Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na Kalonzo Musyoka, akidai kuwa muungano huo unaweza kupatia upinzani nafasi nzuri ya…

Ruto adai Uhuru amekataa handisheki licha ya juhudi zake za kutaka wapatanishwe

HAKUNA siri kwamba uhusiano kati ya Rais William Ruto na mtangulizi wake Uhuru Kenyatta umeharibika. Lakini kiwango cha uhasama kati ya viongozi hao wawili, ambao wakati mmoja walionekana kuwa washirika wasioweza kutenganishwa, unaonekana katika juhudi za Rais Ruto za miaka minne zilizolenga kurejesha uhusiano wao. Katika mahojiano ya kipekee na Taifa Jumapili katika Ikulu ya Nairobi Ijumaa,…

Mke wa Besigye aomba kesi inayomwandama mumewe iahirishwe hadi apate nafuu

MKE wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, Winnie Byanyima, amelaani kuendelea kwa kesi ya mumewe huku mwanasiasa huyo akiwa amelazwa kutokana na hali yake mbaya ya afya. Besigye, 70, anakabiliwa na mashtaka ya uhaini yanayohusiana na madai ya kupanga njama ya kumpindua Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986. Byanyima, ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS,…

Siasa: IEBC yapiga breki kampeni katika maeneo ya ibada, mazishini

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imewapa wanasiasa na wanaowania nyadhifa mbalimbali waliochapisha mabango ya kampeni yenye nembo ya tume hiyo siku tano kuyaondoa mara moja, ikiongeza juhudi za kukabiliana na kampeni za mapema kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Agosti 10, 2027. Katika taarifa kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo, IEBC ilisema matumizi ya nembo yake […]

Azma ya Omar kuwania ugavana Mombasa yaleta mgawanyiko kati ya UDA na ODM Pwani

TANGAZO la Katibu Mkuu wa UDA, Hassan Omar kuwania ugavana Mombasa mwaka 2027 limezua mgawanyiko katika ushirikiano unaoibuka kati ya UDA na ODM, huku juhudi za kugawana maeneo ya kisiasa Pwani zikikabiliwa na changamoto. Bw Omar ametangaza kuwa ataendelea na azma yake ya kuwania kiti hicho, hatua inayotishia mpango wa vyama hivyo kuepuka kushindana moja kwa moja katika baadhi ya kaunti. Kwa zaidi…

Gachagua ataka FBI ichunguze ajali ya ndege iliyomwangamiza Ng’eno

ALIYEKUWA Naibu Rais, Rigathi Gachagua ametaka maafisa kutoka Scotland Yard ya Uingereza na Shirika la Upelelezi la Amerika (FBI) waalikwe nchini kuchunguza ajali ya helikopta iliyomuua aliyekuwa Mbunge wa Emurua Dikirr Johana Ng’eno na watu wengine watano. Bw Gachagua alisema Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kenya (KCAA) haziwezi […]

Walinzi wa Nassir wadaiwa kufyatulia vijana risasi

WATU watatu walijeruhiwa baada ya walinzi wanaodaiwa kuwa wa Gavana wa Mombasa, Abdulswamad Nassir kufyatua risasi katika hafla ya umma katika Uwanja wa Bomu, Changamwe, Mombasa, Ijumaa alasiri. Tukio hilo lilitokea wakati wa mkutano wa kuhamasisha wananchi kuhusu mpango wa Biashara Mtaani, unaoendeshwa kupitia Hazina ya Mzunguko ya Kaunti ya Mombasa kwa wakazi wa Changamwe na Jomvu. Kamanda wa…

Ajabu mapanga sasa yakigeuzwa silaha kali ya wahuni

MAPANGA yanabadilishwa kutoka zana ya kawaida ya shambani kuwa silaha ya kutisha na kuwashambulia watu, huku ripoti ya kijasusi ikifichua kuwa angalau mapanga 500 yalisambazwa kwa vijana waliozua vurugu wakati wa ziara ya Linda Mwananchi, Homa Bay. Huku joto la kisiasa likipanda kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027, vijana wanaobeba mapanga katika mikutano ya hadhara na makabiliano ya kisiasa wamekuwa…

Athari za dawa za kufisha ganzi wakati wa kujifungua kwa upasuaji

KWA Atieno, kumbukumbu ya siku aliyomkaribisha kifungua mimba wake duniani haikujumuisha tu furaha ya kumwona mwanawe, bali pia hofu aliyokuwa nayo kabla ya kujifungua kwa upasuaji (Caesarean Section). Alipofahamishwa kuwa angelazimika kujifungua kwa upasuaji, jambo lililomtisha zaidi halikuwa upasuaji wenyewe bali sindano ya kufisha ganzi inayodungwa kwenye uti wa mgongo. Alikuwa amesikia kutoka…

Wakazi wataka maisha bora baada ya ujangili kuzimwa mpakani

KWA zaidi ya miongo mitatu, wakazi wa Lorogon, mpakani mwa Turkana na West Pokot, wameishi kwa hofu ya majangili wenye silaha. Lakini sasa bunduki zimetulia kwa kiasi kikubwa kufuatia operesheni ya serikali ya kuwapokonya silaha wahalifu hao, na wakazi wanataka amani hiyo iwaletee ajira, maji, umeme na maisha bora. Lorogon iko kati ya Mto Turkwel na vilima vyenye mabonde magumu kufikika, ambayo…

Maafisa waagizwa kupigia debe mafanikio ya serikali kuelekea 2027

SERIKALI ya Rais William Ruto imeanza kuimarisha kampeni ya mawasiliano kwa umma kuhusu sera, miradi na mafanikio yake huku uchaguzi mkuu wa 2027 ukikaribia. Hatua hiyo inafuatia barua ya Mkuu wa Utumishi wa Umma na Wafanyakazi wa Ikulu, Felix Koskei, kwa mawaziri, makatibu, msemaji wa serikali na wakuu wa mashirika ya serikali. Katika barua iliyoandikwa Agosti 17, 2026, Bw Koskei aliwaagiza…

Faili ya uchunguzi wa mlinzi wa Katibu Fikirini Jacobs yafungwa

MAHAKAMA ya Makadara imefunga faili ya uchunguzi dhidi ya mlinzi wa Katibu wa Masuala ya Vijana, Fikirini Jacobs kuhusu kupigwa risasi na kuuawa kwa kiongozi wa vijana mtaani Kariokor, Cecil Ouma, huku ikisubiri uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP). Mahakama ilisema faili hilo haiwezi kuendelea kuwa wazi kusubiri wachunguzi kukamilisha mchakato wa kuwasilisha ripoti ya uchunguzi wa…

Afisa wa polisi aliyeuawa Homa Bay alikuwa akisubiri kupandishwa cheo

KONSTABO Jim Richardson Onkundi, aliyefariki baada ya kupigwa na jiwe wakati wa mkutano wa Linda Mwananchi Homa Bay, alikuwa akisubiri kupandishwa cheo kuwa koplo. Onkundi, 36, alikuwa akiendesha gari la polisi lililokuwa limewabeba maafisa watano kutoka Kituo cha Polisi cha Chemelil, Muhoroni, Kaunti ya Kisumu. Alikuwa amemaliza mafunzo ya kupandishwa cheo katika Chuo cha Polisi Kiganjo na…

Mapanga 500 na silaha zingine zilisambaziwa wahuni Homa Bay, polisi wafichua

TAKRIBAN vijana 500 walilipwa kuziba barabara kuwazuia wafuasi wa Linda Mwananchi kuingia Homa Bay wakati wa mkutano wao Jumapili iliyopita, huku polisi wakifichua kuwa mapanga 500 na silaha nyingine zilisambazwa kabla ya ghasia hizo. Ripoti ya kijasusi iliyotayarishwa baada ya polisi kunasa silaha hizo imeibua wasiwasi kuhusu kiwango cha maandalizi yaliyofanyika kabla ya mkutano wa Agosti 16.…

Gachagua aapa kutembea Emurua Dikirr licha ya vitisho

NAIBU Rais Rigathi Gachagua ameapa kutembelea Emurua Dikirr, Narok, leo Ijumaa licha ya vitisho kutoka kwa viongozi wa eneo hilo. Chama chake cha Democracy for Citizens Party (DCP) kimesema Bw Gachagua atatumia ziara hiyo kuwashukuru wakazi waliounga mkono chama hicho katika uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika hivi majuzi. Pia, anatarajiwa kuzungumzia masuala ya ardhi na kile anachodai ni…

Bunge lapitisha sheria kutatua msongamano shule za kitaifa

SHULE za jamii, zilizo katika kundi la C4, huenda zikanufaika pakubwa na mpango mpya wa usajili wa wanafunzi wa Gredi 10 unaopendekezwa kuanza Januari 2027. Wabunge wamepitisha kwa kauli moja hoja inayotaka Wizara ya Elimu, kwa ushirikiano na taasisi nyingine, kuweka idadi ya mikondo ambayo kila kundi la shule linaweza kuwa nayo. Chini ya pendekezo hilo, shule za kitaifa zilizo kundi la C1…

MAONI: Tuzoee kama nchi kukubali maoni na mitazamo kinzani

KADRI uchaguzi mkuu unavyojongea ndivyo tabia ya kufadhaisha isiyoruhusu mtazamo na msimamo tofauti inavyozidi kujitokeza. Katika taifa linalojivunia demokrasia na utawala wa kikatiba, ungetarajia sote tunafahamu kila mwananchi, awe raia wa kawaida au kiongozi, amehakikishiwa kufurahia haki na uhuru kikatiba mradi hatoingilia uhuru na haki za mwananchi mwenzake. Ni kinaya kuwaona watu mashuhuri…

Mundubile kupinga ushindi wa Hichilema mahakamani

LUSAKA, Zambia: KIONGOZI wa upinzani Zambia, Brian Mundubile, Alhamisi alisema atapinga matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 13 kortini, akidai kuwa kulikuwa na udanganyifu na ukiukaji mkubwa wa haki. Mundubile alisema Jumatano jioni kuwa kampeni yake imekusanya ushahidi wa kasoro katika mchakato wa uchaguzi, kuhesabiwa kwa kura, kutumwa kwa matokeo na kutangazwa kwake. “Kampeni yetu…

Kenya kuagiza magunia milioni 25 ya mahindi ukame ukipunguza uzalishaji

KENYA inapanga kuagiza magunia milioni 25 ya mahindi ili kuziba pengo la nafaka hiyo lililosababishwa na ukame unaoendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini yanayotegemewa kwa uzalishaji wake. Kwenye mahojiano ya kipekee na Taifa Leo Dijitali, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Mutahi Kagwe, alisema uagizaji huo utafanywa na sekta binafsi. “Ni sekta binafsi itakayonunua mahindi.…

Mkuu wa runinga ya Telemundo, mkuu wa Ujasusi Ecuador miongoni mwa 7 waliofariki ajali ya helikopta

WATU saba walioangamia katika ajali ya helikopta Mlima Ololokwe, Samburu walijumuisha Mkenya, Waamerika watano na raia wa Ecuador. Waliofariki wanajumuisha rubani Mkenya na mkurugenzi wa kampuni ya African Heli Adventures Josh Outram, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Ujasusi cha Ecuador Michele Sensi-Contugi na mkewe Stephany Hollihan Yeaza. [caption id="attachment_191376" align="alignnone"…

Binti aonya mamake akome kuchekacheka na mume wake

KATIKA tukio lisilo la kawaida,msupa mmoja wa hapa alimpigia mamake simu na kumuonya vikali akome kucheka cheka na mumewe kila mara. Mwanadada huyo alishuku kwamba wawili hao walikuwa kwenye uhusiano wa kisiri baada ya jamaa kutoa usemi kwamba mama-mkwe alikuwa amedumisha urembo wake. Matamshi hayo yalimshtua mwanadada huyo aliyehisi kwamba mumewe alikuwa na lengo la kunyemelea mama mkwe. Demu…

Wanafunzi wengi wa Gredi 9 hawawezi kusoma ipasavyo -Ripoti

TAKRIBAN thuluthi moja ya wanafunzi wanaojiunga na Sekondari Pevu kutoka Sekondari Msingi hawana ujuzi muhimu wa kusoma, kuandika na kuhesabu, ripoti mpya imefichua. Ripoti hiyo iliyotolewa na Usawa Agenda, shirika linalofanya utafiti kuhusu elimu ya msingi, pia imeonyesha kuwa wanafunzi katika shule za umma za maeneo ya mashambani ndio walioathirika zaidi. Utafiti huo uliofanywa katika kaunti…

Benki ya Equity yaripoti kuvuna faida kemkem ikielezea kuimarika sekta ya mikopo na akiba

EQUITY Group Holdings imeripoti ongezeko la asilimia 32 la faida baada ya ushuru katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, ikiashiria kuimarika kwa biashara yake nchini Kenya na katika matawi yake ya kikanda. Benki hiyo ilisema jana faida baada ya ushuru ilipanda hadi Sh45.5 bilioni kutoka Sh34.6 bilioni katika kipindi kama hicho mwaka jana. Faida kabla ya ushuru iliongezeka kwa asilimia 39 hadi…

Mwanamume kulipa mpenziwe wa zamani Sh2.5m baada picha za siri kusambaa mitandaoni

MAHAKAMA Kuu imeamuru mwanamume mmoja kumlipa Sh2.5 milioni mwanamke aliyeolewa baada ya picha zake za uchi kusambaa mtandaoni, ikisema mtu anayemiliki picha za siri za mwingine ana wajibu wa kuzilinda. Mahakama ilisema kutozuia picha hizo kusambazwa bila idhini kunaweza kumfanya mhusika kuwajibika, hata kama mwathiriwa hawezi kuonyesha moja kwa moja akaunti iliyozichapisha. Mwanamume huyo, GH,…

Wataalamu waeleza kwa nini kuna baridi kali Nairobi mwezi huu wa Agosti

KWA Wakenya wengi, Agosti umekuwa mwezi wa kuvaa nguo nzito, kujifunika blanketi na baridi kali isiyo ya kawaida asubuhi. Nairobi na maeneo ya nyanda za juu katikati mwa nchi yamekuwa yakishuhudia hali hiyo hadi mchana, jambo linalowafanya wengi kujiuliza ni kwa nini ilhali msimu wa kiangazi unakaribia kufika mwisho. Lakini wataalamu wa masuala ya hali ya hewa wanasema baridi ya Agosti si jambo…