Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Umuhimu wa bima ya afya kwa wasafiri ni pamoja na kupunguza gharama kwa taifa mwenyeji haswa wakati huu nchi nyingi hususan za Afrika zinashuhudia ongezeko la milipuko wa magonjwa ya milipuko Sharti hilo pia linatoa fursa kwa nchi kuboresha mifumo ya afya ili kukidhi mahitaji ya wasafiri wanaohitaji huduma za afya kwa nchi wanazozitembelea.
Imani kuwa mama na mtoto wanapotenganishwa inaweza kuathiri ubora wa maziwa ya mama inapotosha. Watalaam wanasisitiza maziwa ya mama hayawezi kuharibika kwenye titi. Aidha kunyonyesha kwa uaminifu kunaweza kukuepusha na saratani na mbinu pia ya kupanga uzazi.
Maumivu wakati msichana au mwanamke anapokuwa kwenye siku zake za hedhi, yanaweza kuwa ya kawaida ila maumivu haya yanapomfanya kushindwa na shughuli za kawaida si kawaida Dkt Dominic Osiemo anasema maumivu haya makali yanaweza kuwa dalili za baadhi ya changamoto za kiafya kama vile Uvimbe au ugonjwa wa Endometriosis.
Raia mmoja wa Kenya amefika kwenye bunge la kitaifa nchini Kenya akitaka swala la wanaume na wanawake kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa kuorodheshwa kuwa ulemavu Kwa mujibu wa daktari Dominic Osiemo ,tatizo hilo linachangiwa na maswala kadhaa yakiwemo matumizi ya dawa za kisukari ,shinikizo la damu na msongo wa mawazo.
Kaunti ya Turkana inaongoza nchini Kenya kwa visa vya watu kung'atwa na nyoka. Wataalamu wa afya wanasema mabadiliko ya tabianchi, joto kali na changamoto za upatikanaji wa huduma za afya vinaongeza hatari kwa wakazi wa maeneo mengi ya kaunti hiyo,huku shirika la afya duniani WHO likisema visa vya kuumwa na nyoka vinapuuzwa wakati huu karibia watu 32000 wakifariki kila mwaka kutokana na sumu ya…
Mashirika ya kiraia yanasema nchi za Afrika zinalipa deni na kuachwa na kiasi kidogo cha pesa kuendesha shughuli muhimu za serikali ,sekta ya afya ikiathirika zaidi Mashirika haya yanataka umoja wa Afrika kuja na jopo ambalo litakuwa linaangazia maswala yote kuhusu mikopo ili kupunguza dhulma kwa nchi zinazoendelea
Tafiti kadhaa za kiafya zimebainisha magonjwa mengi yasiyoambukizwa yana uhusiano mkubwa na vyakula vilivyosindikwa na hali ya watu kukosa kuzingatia mazoezi ya kila mara. Kenya ikiwa taifa la kwanza Afrika Mashariki kupitisha mwongozo unaotoa maelekezo kuhusu viwango vya madini ambavyo vyakula au vinywaji vinavyouzwa vinafaa kukidhii au kwa lugha ya kiingereza Kenya Nutrient Profile Model,sasa…
Mwezi Juni ni mwezi wa kutoa uhamasisho kuhusu afya ya akili miongoni mwa wanaume ,swala la afya ambalo hupuuzwa mno Daktari Dominic Osiemo anasema wanaume wana haki wa kuonesha hisia ,kueleza maumivu yao na kutaka kuskizwa. Na wanapofanya hivyo wanalinda afya zao za akili. Anaonya wanaume wengi wanakuwa hatarini kwa sababu wanajaribu kudhihirishia jamii kuwa wao ni imara siku zote. Baadhi ya…
Katika mkakati wa kupunguza unyanyapaa kwa wazazi wanaowalea watoto wenye Autism shule ya Mali inatoa tiba nasaha na elimu kwa pamoja ikizingatia pia mahitaji ya wazazi wao ambao mara nyingi wanahitaji pia matunzo
Shinikizo zinazidi kutolewa kwa mataifa ya Afrika kukumbatia sera za uchukuzi zilizo salama na endelevu ili kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na barabara na madhara ya ajali za barabara kwa jamii. Katika kongamano la kujadili mpango huo wa usalama ulio endelevu ,wadau wamesikitika vifo vya barabarani bado vinaripotiwa miongoni mwa watembea miguu na waendesha pikipiki. Katika makala ya Siha…
Mataifa ya Afrika yameshuhudia mafuriko katika miaka ya hivi karibuni ,hali ambayo imesababisha wananchi wengi kulazimika kuhama makazi yao Nchini Kenya ,ukanda wa magharibi ,katika eneo la Busia,mafuriko hayo yamevuruga kalenda za wanafunzi wa shule ,watoto wengi wakishindwa kuendelea na shule au kukubaliana na msongamano kwenye shule chache ambazo ziko maeneo salama Hali hii imewasababisha…
Watu 220 wamefariki kwenye mlipuko wa Ebola unaohusishwa na virusi adimu vya Bundibugyo huku wengine zaidi ya 1000 wakiwa wameambukizwa Mlipuko huu hatari umesababisha baadhi ya mataifa kufunga mipaka yake na kuweka masharti magumu ya tahadhari
Baadhi ya makubaliano yalitotangazwa na Ufaransa baada ya siku mbili ya kongamano la Africa Forward ni ufadhili kwa uzalishaji wa dawa na chanjo hapa barani Afrika. Shirika la Unitaid pia lenye ushirikiano na Ufaransa lilitangaza kuratibu mchakato wa kuzalishwa dawa mpya ya kuzuia virusi vya HIV ,Lenacapavir kuzalishwa Afrika Kusini. Na kwenye viungo vingine vilivyosheheni majadiliano ya…
Utafiti unaoangazia vinasaba katika ukanda wa Afrika unaweza kuwa jawabu kwa ubainishaji potovu,gharama ya juu ya matibabu na usugu wa vimelea . Kwa kuanzia , Mashirika matatu ya Afrika ya kitafiti yametangaza mkataba wa dola milioni 3 nukta 5 ambao utawekezwa kwenye utafiti huu wa DNA barani . Mashirika haya yakiwa ni Biolinx Africa, YTO Foundation yenye makao Ivory Coast na Nextgen Molecular Lab…
Ufadhili wa afya ukanda wa Afrika umezidi kupungua tangu kusitishwa kwa ufadhili mkubwa wa kigeni Pengo hilo linamanisha serikali nyingi hazina uwezo wa kifedha wa kutosha kuendelea kutoa mafunzo endelevu ya wahudumu wa afya. Katika kujaribu kutatua changamoto hii ,mpango wa ECHO unaowasaidia wahudumu wa afya kujifunza wakati wanapoendelea kuwahudumia wagonjwa ,umekuja kuleta matumaini.
WHO ilitoa nafasi zaidi kwa mataifa ya ulimwengu kujadililiana zaidi kuhusu vipengee muhimu kwenye mkataba wa kukabiliana na majanga ya kidunia Vipengee hivyo ni pamoja namna mataifa yanaweza kunufaika kutokana na mchango wao kwenye tafiti za kisayansi ,vimelea vinavyotoka kwenye mataifa yao na usawa wakati wa usambazaji wa chanjo au dawa
Asilimia 37 ya vituo vya afya nchini Sudan vimeharibiwa wakati wa mapigano na haviwezi kutoa huduma za afya Shirika la madaktari wasio na mipaka,MSF limekuwa likiwahudumia wagonjwa wenye majeraha ,waathiriwa wa magonjwa ya milipuko na waathiriwa wa ubakaji. Hali ya usalama imeilazimu MSF kusitisha huduma katika maeneo kadhaa baada ya kushuhudiwa mashambulizi ya moja kwa moja kwenye vituo vya afya…
Magonjwa yanayoshambulia kinga yanapompata mtu ,huendelea kusambaa ,kudhuru kingamwili na kumweka hatarini mgonjwa kiasi cha kuwa mgonjwa anaweza kupatwa na magonjwa zaidi ya moja ya aina hiyo. Elwyn Chebet aligunduliwa na Lupus na baadaye akajikuta anapambana na magonjwa zaidi ya tano aina ya Autoimmune. Mwezi Machi ambapo ulimwengu huelekeza kurunzi kwenye magonjwa ya mfumo wa kinga au…
Watalaam wanasema vijana wengi hufikia kwenye maduka ya kuuza dawa kupata huduma za afya baadala ya kufika hospitali kufanyiwa vipimo Unyanyapaa pia inachangia wanaume au vijana kuwa na ari ya kwenda kupata huduma za afya haswa za TB.
Unapopata magonjwa ambayo yanaathiri kinga ya mwili wako,ina maana kuwa kinga yako inaweka mifumo yote ya mwili kwenye hatari. Unaweza kujikuta unapata magonjwa kama Lupus,ugonjwa wa Tezi Koo au Mifupo yako kuwa nyepesi kiasi cha kuvunjika kwa urahisi. Ubainishaji wa magonjwa haya unahitaji subira na ufuatialiaji wa karibu ili kuelewa kila dalili anayoonesha mgonjwa .Gharama yake basi inamanisha…
Siku za hedhi huchukuliwa kuwa swala la wanawake na halifai kuzungumzwa hadharani kwa jamii nyingi .Hali hii imesababisha wanawake na wasichana kupitia unyanyapaa ijapokuwa hili ni swala la haki ya uzazi
Ripoti ya afya akili duniani ,inaonya kuhusu madhara yanayotokana na matumizi ya simu za mkononi miongoni mwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 na 34 Katika mataifa ya Afrika ambapo matumizi ya simu hizi huanza kwa kuchelewa ,vijana walionekana kuwa afadhali ikilinganishwa na mataifa kama Finland ambapo watoto huanza kutumia simu katika umri mdogo mno. Katika mataifa yaliyozingatia maswala ya…