RSS Amplifier

News source

MICHUZI BLOG

Most read Swahili blog on earth

michuzi.co.tzSource feed ↗26 articles

Overdue Last read · last published · next check
Last read 7 hours ago, longer than this feed's 1 hour schedule.

Written by

Latest articles

PROF. NOMBO ATEMBELEA BANDA LA TUME YA TAIFA YA UNESCO MAONESHO YA WIKI YA ELIMU,TANGA

Na Julitha Mlay ,NATCOM KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, ametembelea Banda la Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu Kitaifa yanayoendelea jijini Tanga. Katika ziara hiyo, Prof. Nombo alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Tume hiyo, pamoja na maudhui…

NEEMA: MKONDO WA AMALI WATOA FURSA KWA VIJANA KUJIAJIRI

MWANAFUNZI wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Ufundi Tanga, Neema Bundala akionesha uwezo wake wa kujua mfumo wa nchini unafavyofanya kazi kwenye Banda la NACTVET ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu inayoendelea katika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, jijini Tanga. Na Mwandishi Wetu, Tanga MWANAFUNZI wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Ufundi Tanga, Neema Bundala, amesema…

VETA TANGA YABUNI MASHINE YA KUTOTOLESHEA VIFARANGA 840

MWANAFUNZI wa Chuo cha VETA Tanga , Maria Moshi akizungumza na wananchi waliotembelea Banda la VETA kwenye ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu inayoendelea katika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, jijini Tanga waliotaka kujua mashine ya kutoteleshea vifaranga. Na Mwandishi Wetu, Tanga CHUO cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Tanga kimebuni mashine ya kutotoleshea…

TCAA YAPONGEZWA KWA MABORESHO YA HUDUMA NA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA SEKTA YA ANGA

WAZIRI wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa (Mb) akizungumza katika bamda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) alipotembelea wakati wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Sekta ya Uchukuzi na Usafirishaji, linalofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imepongezwa kwa kuendelea kusimamia sekta ya usafiri wa anga kwa ufanisi na…

VETA KUZALISHA WATAALAMU 400 WAZAWA KATIKA SEKTA YA MADINI

Afisa Uratibu wa Ukuzaji Mitaala wa VETA Mhandisi Audiface Tarimo akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la VETA kwenye Wiki ya Kitaifa ya Elimu,Ujuzi na Ubunifu linalofanyika Shule ya Sekondari Usagara jijini Tanga. Na Mwandishi Wetu, Tanga MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inatarajia kuzalisha wataalamu wazawa wapatao 400 katika sekta ya madini baada ya wataalamu wake…

LST YAANZISHA MFUMO WA KIDIJITALI WA e-FIELD MIS 2026

Na Mwandishi Wetu, Tanga TAASISI ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) imeondoa matumizi ya karatasi kwa wanafunzi wanaofanya mafunzo kwa vitendo sehemu za kazi (field) katika ofisi na taasisi mbalimbali nchini na kuanza kutumia mfumo wa kidijitali wa kusimamia mafunzo hayo unaotambulika kama LST e-FIELD MIS 2026. Hatua hiyo inalenga kurahisisha usimamizi wa mafunzo kwa vitendo…

Kampeni ya Chanjo ya Polio Yalenga Kuwafikia Watoto 207,096 Jijini Dodoma

Na. Mwandishi wetu, DODOMA Wizara ya Afya kupitia Idara ya Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, imewataka wananchi wa Jiji la Dodoma kujitokeza na kuwapeleka watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 kupata chanjo ya matone ya Polio, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuongeza kinga dhidi ya ugonjwa huo. Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Magdalena Dinawi kutoka Wizara ya Afya, Idara ya Kinga, alisema…

KAMATI YA BUNGE YAISHAURI SERIKALI KUONGEZA RUZUKU KWA TBA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeiomba Serikali kuongeza ruzuku kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), ili kuwezesha kuongeza kasi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya watumishi wa umma nchini. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Selemani Kakoso, wakati wa ziara ya kukagua miradi ya nyumba za watumishi inayotekelezwa na TBA katika maeneo ya Kisasa na Nzuguni jijini Dodoma,…

VIJANA TANGA WABUNI TEKNOLOJIA YA KUWAOKOA WAVUVI

Na Oscar Assenga, TANGA Programu ya Tanga Yetu imeendelea kuwa chachu ya maendeleo kwa vijana na watoto wa Jiji la Tanga, kupitia miradi inayolenga kuimarisha elimu, ujuzi, teknolojia na ubunifu kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii. Akizungumza katika Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, Afisa Mawasiliano wa Programu ya Tanga Yetu, Cliford Sangai, alisema programu…

BALOZI SALUM AZITAKA FCC, TBS NA WMA KUPAMBANA NA BIDHAA BANDIA NA DUNI.

Mameneja wa Kanda na Mikoa wa Taasisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Tume ya Ushindani (FCC) pamoja na Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) wameagizwa kuhakikisha hakuna bidhaa bandia na duni katika maeneo yao wanayoyasimamia kiutendaji. Maelekezo hayo yametolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhe. Balozi Waziri Rajab Salum, wakati wa kikao cha menejimenti za Tume ya Ushindani…

GH Tanzania Yaadhimisha Miaka 15 ya Utumishi Kazini kwa Maafisa Wakaguzi na Askari.

Maafisa Wakaguzi na Askari wa intake ya 20211/2012 maarufu kwa jina GH Tanzania wanatarajia kuadhimisha miaka 15 ya utumishi wao kazini katika hafla ambayo itakayofanyika Jumamosi, Agosti 22, 2026, katika Shule ya Msingi Mitindo, Misungwi mkoani Mwanza. Maadhimisho hayo yanatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya kutathmini safari ya miaka 15 ya utumishi, huku yakilenga kuimarisha mshikamano, upendo na…

WAZIRI KAIRUKI AZINDUA AWAMU YA PILI YA FAIBA MLANGONI KWAKO, ATOA MAELEKEZO MANNE KWA TTCL

Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, ametoa maelekezo manne kwa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), akilitaka kuhakikisha Awamu ya Pili ya Mradi wa Faiba Mlangoni Kwako (Fiber to the Home – FTTH) inawanufaisha wananchi kwa kuwapatia huduma yenye ubora, uhakika na gharama nafuu. Waziri Kairuki ametoa maelekezo hayo…

RC BURIAN ATOA MWELEKEO KWA WANANCHI 66 WA MSAKANGOTO

Na Oscar Assenga, MUHEZA MKUU wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, amewataka wananchi 66 wa Kitongoji cha Bago Maisha Plus ,Kijiji cha Msakangoto, Kata ya Kigombe wilayani Muheza, kuondoka katika eneo walilokuwa wakiishi na kuhamia eneo jipya lililotengwa na Serikali ya Kijiji, huku akiahidi kuwa Serikali itaendelea kuwasaidia katika kipindi cha mpito. Wananchi hao wamekumbwa na…

TANZANIA, UBELGIJI KUIMARISHA BIASHARA NA UWEKEZAJI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ubelgiji nchini Tanzania, Mhe. Lot Debruyne, katika Ofisi Ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam. Baada ya makabidhiano hayo, viongozi hao wamejadili namna ya kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano kati ya…

SIMANJIRO WAJIPANGA KUSHIRIKI MANYARA TANZANITE MARATHON 2026

Na Mwandishi wetu, Simanjiro MADIWANI, watumishi na baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanashiriki kwa wingi mbio za Manyara Tanzanite Marathon 2026 zinazotarajia kufanyika mjini Babati. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Kaleya Melita Mollel akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani amesema wamejipanga ipasavyo kushiriki…

SUZA YATUMIA TAFITI KUTATUA CHANGAMOTO ZA JAMII.

Na Belinda Joseph – Tanga CHUO Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimeeleza namna tafiti zinazofanywa na chuo hicho zinavyolenga kutatua changamoto za wananchi na kuchochea maendeleo ya Taifa, ikiwemo sekta ya uvuvi na madini. Akizungumza katika Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu inayoendelea Tanga, Makamu Mkuu wa SUZA, Prof. Said Ali Hamad Vuai, amesema chuo hicho kinafanya utafiti wa…

BODI YA TAFICO YARIDHISHWA KUKAMILIKA KWA BANDARI YA UVUVI KILWA MASOKO

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), imefanya ziara ya ukaguzi katika mradi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko, kwa lengo la kujionea hatua ya utekelezaji wa mradi, kukagua miundombinu na maandalizi yaliyofanyika kuelekea kuanza kwa matumizi ya bandari hiyo, pamoja na kutathmini fursa zitakazotokana na uwekezaji huo katika shughuli za uvuvi na uchumi wa buluu. Ziara hiyo…

NeST YAUNGANISHA MIFUMO 30+, YARAHISISHA ZABUNI NA KUDHIBITI NYARAKA ZA KUGHUSHI

Na Janeth Raphael – MichuziTv Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST) umeendelea kuimarishwa kwa kuunganishwa na zaidi ya mifumo 30 ya taasisi mbalimbali, hatua inayolenga kurahisisha mchakato wa zabuni za umma, kuongeza ufanisi na kuimarisha uhakiki wa taarifa za wazabuni. Hatua hiyo pia imeongeza uwezo wa Serikali kudhibiti matumizi ya nyaraka zisizo halali katika mchakato wa ununuzi wa…

WRRB YATAKIWA KUONGEZA ELIMU KUCHOCHEA MATUMIZI YA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA

Na.Mwandishi Wetu- Dodoma KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imeipongeza Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yake na kuitaka kuharakisha matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala (WRS) katika zao la parachichi ili kuongeza tija kwa wakulima. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Deodatus Mwanyika, ametoa pongezi hizo leo Agosti…

WAZIRI WA ARDHI DKT AKWILAPO AINGIA ‘SITE’ KUTAFUTA SULUHU YA MIGOGORO YA ARDHI MKOANI TANGA

Na Munir Shemweta,Tanga Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo, amefanya ziara katika maeneo yenye migogoro ya ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Tanga na Halmashauri ya Mji Handeni mkoani Tanga, kwa lengo la kupata undani wa migogoro hiyo baada ya kupokea malalamiko. Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya…

Serikali: Mashindano ya Ujuzi Yaandaa Vijana Kushindana Kimataifa

Na Mwandishi Wetu, Tanga SERIKALI imesema mashindano ya ujuzi na ubunifu ni sehemu ya mkakati wa kuwaandaa vijana wenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira na kuwawezesha kushindana katika majukwaa ya kimataifa. Hayo ameyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo, wakati akizungumza katika Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu inayoendelea jijini Tanga.…

WADAU WATAKIWA KUTUMIA INTANETI KUJENGA JAMII, ISITUMIKE KUENEZA CHUKI, MATUSI

Na Mwandishi Wetu WADAU wa teknolojia na usimamizi wa intaneti wametakiwa kutumia fursa zinazotokana na mtandao huo kwa maendeleo ya jamii badala ya kuutumia kwa matusi, chuki, udhalilishaji na vitendo vinavyoweza kuathiri maslahi na haki za watu wengine. Rai hiyo imetolewa na Mratibu wa Tanzania Internet Governance Forum (TIGF), Dkt. Nazarius Kirama, wakati wa Mkutano wa 13 wa Jukwaa la Usimamizi…

KONGAMANO LA 5 LA KIMATAIFA LA UCHUMI WA BULUU KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Prof. Tumaini Gurumo, amesema maandalizi ya Kongamano la 5 la Kimataifa la Uchumi wa Buluu yanaendelea vizuri. Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 7 hadi 9 Septemba 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, huku washiriki kutoka zaidi ya nchi saba wakitarajiwa kuhudhuria. Akizungumza na waandishi wa…

SEKIBOKO: VIJANA GEUZENI UJUZI KUWA AJIRA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Husna Sekiboko, ametoa wito wa kuimarishwa kwa elimu na mafunzo ya ufundi na ujasiriamali nchini, akisema ujuzi wa vitendo unaweza kuwa silaha muhimu kwa vijana katika kukabiliana na ukosefu wa ajira kwa kujiajiri na kuunda ajira kwa wengine. Amesema hayo akiwa kwenye banda la VETA katika Maadhimisho ya Wiki ya…

KATIBU MKUU NOMBO AAGIZA TAEC KUONGEZA ELIMU YA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA KWA WATANZANIA

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, ameiagiza Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) kuongeza elimu kwa umma kuhusu matumizi ya teknolojia ya nyuklia, ili Watanzania waelewe manufaa yake na matumizi chanya katika maisha na maendeleo ya taifa. Prof. Nombo ametoa agizo hilo Agosti 20, 2026 jijini Tanga alipotembelea banda la TAEC katika Maonesho ya Wiki ya…

RC MANYARA AISHAURI TMDA KUIMARISHA UTOAJI ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU MATUMIZI SAHIHI DAWA,VIFAA TIBA

NA EMMANUEL MASSAKA MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imeshauriwa kuendelea kuimarisha utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya dawa na vifaa tiba. Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Bi. Queen Sendiga alipokuwa akifungua kikao cha siku mbili kati ya TMDA, wahariri na waandishi wa habari kutoka mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro, kilichofanyika mkoani Manyara.…