Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
Tuliyoangazia leo ni pamoja na uchambuzi wa matokeo na matukio ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada inayofikia tamati wikendi hii, mechi za kufuzu kombe la dunia la basketboli chini ya miaka 18, Kenya yawasilisha nia ya kuandaa mashindano ya dunia ya riadha 2029. Je, Yanga itatetea ubingwa wa ligi kuu Tanzania baada ya kushinda ngao ya jamii?, PSG yashinda taji la UEFA Super Cup, tetesi za…
Tumeangazia uchambuzi wa matokeo na matukio kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika kina dada inayoingia kwenye mtoano, droo ya michuano ya klabu bingwa, CAF yamuunga mkono rais Infantino, Rayon yashinda ubingwa CECAFA baada ya miaka 28, Simba Day ni leo, mshindi wa medali ya fedha mbio za kutembea mita 10,000 kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola 2026 Stephen Ndangiri apigwa marufuku kwa tuhuma za…
Leo kwenye kipindi tunaangazia WAFCON inayoendelea nchini Morocco - Kenya yaaga mashindano huku Tanzania ikisalia na matumaini lakini Nigeria na Afrika Kusini zimeanza kwa kusuasua, wanariadha wanaendelea kunyakua medali katika mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Scotland, wakati mashindano ya Cecafa Kagame Cup yakiingia nusu fainali.
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na kuanza kwa mashindano ya kina dada ya Afcon, Kombe la Cecafa, mashindano ya Jumuiya ya Madola, tetesi za uhamisho Ulaya na Afrika Mashariki, mahakama ya kutatua migogoro duniani kuskiza kesi ya kubaini bingwa wa Afcon 2025 mwezi Oktoba tarehe nane.
Tuliyokuandalia leo ni pamoja uchambuzi wa nusu fainali, mechi ya mshindi wa tatu na taarifa kuu kuhusu Kombe la Dunia kuhusu washindi kutuzwa pete pamoja na medali na kombe huku Ballon d'Or yatangaza mchezaji anayecheza nje ya Ulaya ana uwezo wa kushinda tuzo hiyo. Timu ya taifa ya kina dada ya Kenya na Tanzania zasafiri kwa ajili ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Morocco, fainali ya Congo Cup…
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na uchambuzi wa raundi ya 16 bora na robo fainali michuano ya Kombe la Dunia, Misri na Morocco zikiaga mashindano, Mbappe na Messi wang'ang'ania kiatu cha dhahabu, Yanga yapata kocha mpya Manqoba Mngqithi kutoka Afrika Kusini, Emmanuel Wanyonyi avunja rekodi ya mita 1000m mashindano ya Diamond League, mchezo mpya wa Flag Football waendelea kukua na kupata umaarufu…
Tuliyokuandalia leo ni mkusanyiko wa matukio ya raundi ya 32, je ni wakati timu changa kuanza kutamba? Timu mbili tu za Afrika kati ya tisa zafuzu kumi na sita bora, nini kimeiponza Afrika? uchambuzi wa raundi ya 16 bora inaanza leo, kiatu cha dhahabu na mechi za kufuzu Kombe la Dunia la wasichana chini ya miaka 17. Yanga yashinda ubingwa wa Tanzania kwa mara ya 32 huku DRC ikifuzu raundi ya pili…
Hatua ya makundi kwenye Kombe la Dunia inafikia kilele hii leo, ni timu gani zimefuzu hatua ya mtoano? Wiki ya pili ya michuano hii imeshuhudia rekodi zikiwekwa na kuvunjwa huku mataifa ya Afrika yakiendelea kufanya vizuri zaidi, lakini pia tutakupa uchambuzi wa mechi za kesho asubuhi. Aidha tumeangazia michuano ya Afrika Mashariki mchezo wa Baseball, tetesi za uhamisho na mashindano ya Paris…
Leo tumeangazia kwa undani matukio na matokeo yote ya wiki ya kwanza michuano ya Kombe la Dunia 2026 - Mbappe, Messi waweka historia wakati Cape Verde na DRC zikihangaisha miamba wa soka wa ulaya, Tunisia yamfuta kazi kocha, uchambuzi wa mechi za leo. Aidha ni mwaka mmoja kuelekea Kombe la Mataifa ya Africa 2027, matokeo ya tenisi kombe la Davis Cup, Police fc ya Rwanda yamfuta kazi kocha wake,…
Tumeangazia Kombe la Dunia 2026 kuanza kwa vikwazo kadhaa, raia wa Afrika waiunga mkono Mexico dhidi ya Afrika Kusini, uchambuzi wa mechi ya leo Brazili dhidi ya Morocco, DRC wakijiandaa kupambana na Ureno wiki ijayo, maandalizi ya mbio za Kigali Marathon zakamilika, klabu ya Gor Mahia nchini Kenya yaamrishwa kufanya uchaguzi upya,
Tuliyokuandalia leo ni mambo muhimu ya kufahamu kuelekea Kombe la Dunia, timu ya Iran na mwamuzi wa Somalia hatimaye wapokea visa zao, namna mataifa ya Afrika yamecheza kwenye mechi za kirafiki kuelekea Kombe la Dunia, Riquelme na Florentino kupambania urais wa Real Madrid, Kenya kuandaa Davis Cup, kocha wa Kenya ajitetea baada ya sare dhidi ya Lesotho, tuzo za Ligi Kuu Kenya, kocha Flaurent…
Leo tumeangazia Arsenal kushinda ubingwa wa Ligi Kuu baada ya miaka 22, kocha wa Uingereza Tuchel azomewa kuwaacha nje wachezaji kadhaa, kocha wa DRC Desabre ataja kikosi cha Kombe la Dunia, Aston Villa yashinda Kombe la Europa, Droo ya kufuzu michuano ya AFCON 2027 yakamilika huku AFCON U17 ikiendelea, fainali za BAL zaanza Kigali, Kipchoge kukimbia marathon ya kwanza Afrika, Motsengo Omba…
Leo tunaangazia baadhi ya matukio ya michezo yaliyozungumziwa kwenye mkutano wa Africa Forward Summit uliokamilika hiki hii, uchambuzi wa Ghana kukosolewa kuandaa mashindano duni ya Afrika ya riadha, Al Hilal ya Sudan yatwaa ubingwa wa soka Rwanda, Motsengo Omba akizindua nguzo zake tano za uongozi wa Fecofa, fainali ya Kombe la Shirikisho, Afcon U17 yaanza huko Morocco, mataifa yaanza kuzindua…
Tuliyokuandalia leo ni kufutwa kazi kwa kocha wa Yanga Pedro Goncalves, wawaniaji wengine wawili wajiondoa uchaguzi wa urais DRC, mashindano ya magari ya Africa yangoa nanga nchini Uganda, fainali ya Kombe la Shirikisho mkondo wa kwanza kupigwa leo usiku, mechi za kufuzu Kombe la Dunia la wasichana chini ya miaka 20, FIFA imetoa orodha ya wasanii wa kutumbuiza mechi za ufunguzi Kombe la Dunia,…
Leo tumeangazia mashindano ya kwanza kabisa ya kina dada ya FIFA Series inayoandaliwa nchini Kenya, timu tano zimetinga mchujo wa ligi kuu, ziara ya rais wa CAF Motsepe nchini Senegal, ligi ya mabingwa Afrika yaingia hatua ya nusu fainali, kocha Aliou Cisse atua nchini Angola, michuano ya kufuzu Kombe la Dunia la wasichana chini ya miaka 17, droo ya Afcon U17, michuano ya shule za upili za Afrika…
Leo tumeangazia kufuzu kwa DRC michuano ya kombe la dunia tukiwa na mgeni wetu Felly Mulumba, mchezaji wa soka kutoka DRC, Ghana yamfuta kocha Otto Addo, mageuzi katika kamati andalizi ya AFCON 2027 nchini Kenya, Tigers na Petro de Luanda zafuzu fainali ya BAL, Algeria mabingwa wa basketboli ya vitimagu Afrika, kustaafu kwa Victor Wanyama huku ligi ya Kenya ikilenga kuwa bora Afrika, je De Zerbi…
Leo kwenye jukwaa tumeangazia rufaa ya Senegal kwa mahakama kuu ya spoti, ripoti ya CAF yasema Afrika Mashariki haipo tayari kuandaa Afcon 2027, Afrika Kusini na Kenya zafuzu Kombe la Dunia la gofu ya chipukizi, ripoti maalum ya FIFA Series mjini Kigali, mashindano ya KipKeino Classic yapata sura mpya, ni kwa nini Djigui Diarra amepigwa marufuku ya mechi tatu nchini Tanzania?, vikwazo vipya vya…
Leo kwenye kipindi tunaangazia hisia za baada ya Caf kuivua Senegal ubingwa wa Afrika, kwenye tenisi Kenya na Ufaransa zimeingia kwenye ushirikiano, hatma ya Kenya kaundaa Afcon 2027, FIFA yaweka vikwazo kwa Nigeria na DRC, robo fainali ligi ya klabu bingwa Afrika kuanza leo, DRC yashindwa ubingwa wa dunia kwenye basketboli ya vitimagu, ushirikiano wa FIFA na YouTube, Ronaldo kukosa mechi za…
Mashindano ya dunia ya kukimbiza Magari, Kenya Safari Rally, yanaendelea kushika kasi mjini Naivasha ambapo madereva mbalimbali duniani, wanachuana kutafuta ubingwa. Nani ataibuka bingwa ?
Kwenye kipindi cha leo tumeangazia kuondoka kwa kocha mkuu wa Morocco Walid Regragui, Burkina Fason yapata kocha mpya, athari ya kuahirishwa kwa michuano ya WAFCON, vikwazo vya CAF dhidi ya Al Ahly, Faith Kipyegon aorodheshwa kwa mara ya tatu kuwania tuzo ya dunia ya Laureus. FIFA yatangaza sheria mpya za soka kuelekea Kombe la Dunia. Fred Kerley apigwa marufuku ya miaka miwili. Je, ni suala la…
Mkenya Njoroge Kibugu alifuzu mchujo wa mashindano ya dunia ya gofu ya Magical Kenya Open wakati mnyarwanda Celestin Nsazuwera akiweka historia, uchambuzi wa droo ya michuano ya klabu bingwa Afrika, mashindano ya wanawake ya COSAFA, wakenya wang'ara katika michuano ya fencing ya Afrika, TFF yafungua zabuni ya haki za kamari katika debi la kariakor, Fifa kufadhili ujenzi wa viwanja vya soka huko…
Leo tumeangazia CAF kudhibitisha kuwa AFCON 2027 itaandaliwa Afrika Mashariki licha ya tetesi za kuahirishwa au kuhamishwa, uchambuzi wa raundi ya mwisho ya hatua ya makundi mechi za klabu bingwa, mechi za kufuzu kombe la dunia la wasichana U20, siku ya kwanza ya michuano ya raga ya wachezaji saba kila upande divisheni ya pili ya HSBC, mfumo mpya wa mashindano ya Tour du Rwanda, kiungo wa Ghana…
Leo tumeangazia mechi za klabu bingwa Afrika, Yanga itachuana na FAR Rabat nayo Azam ikicheza na Maniema, matukio kuelekea michuano ya gofu ya Magical Kenya Open, mechi za kufuzu kombe la dunia la kina dada chini ya miaka ishirini, rais wa soka DR Congo asimamisha shughuli zote katika uwanja wa Tata Raphael, Rais wa FIFA Infantino asema marufuku dhidi yz Urusi hayajasaidia chochote, mzozo kati ya…