Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
Msikilizaji katika mazingira ambayo migogoro na changamoto za kiuchumi zimeathiri maisha ya kila siku ya wananchi, wanawake wengi wamekuwa wakitafuta njia mbadala za kujipatia kipato na kuendesha familia zao.Hali hii inashuhudiwa katika mji wa Goma, mashariki mwa DRC, ambako baadhi ya wanawake wamegeukia ufugaji wa kuku kama njia ya kujikimu, hasa baada ya shughuli za baadhi ya taasisi za kifedha…
Msikilizaji taifa linaweza kuishi siku moja baada ya nyingine bila kujua linaelekea wapi. Lakini taifa linalotaka kujenga uchumi imara, ajira bora na maisha bora kwa wananchi wake, linahitaji zaidi ya mipango ya leo, kwa kifupî linahitaji dira. Kwenye makala ya wiki hii tunaangazia dira ya taifa ni nini.
Mara kadhaa tumesikia serikali zetu zikitangaza kuwa zinauza hati fungani za Serikali za muda mfupi na muda mrefu, yaani Government Bonds na Treasury bill, serikali zikikusanya mabilioni ya fedha kutoka kwa wawekezaji. Sasa je, hatifungani ni nini? Je, mwananchi wa kawaida anaweza kuwekeza?
Mara kadhaa tumesikia serikali zetu zikitangaza kuwa zinauza hati fungani za Serikali za muda mfupi na muda mrefu, yaani Government Bonds na Treasury bill, serikali zikikusanya mabilioni ya fedha kutoka kwa wawekezaji. Sasa je, hatifungani ni nini? Je, mwananchi wa kawaida anaweza kuwekeza?
Katika Makala haya hivi leo tunajadili uhusiano kati ya siasa za kimataifa na uchumi wa wananchi wa Afrika, mara yingi tunasikia taarifa za vita, migogoro ya kisiasa au mivutano kati ya mataifa makubwa kama Urusi na Ukraine, Mashariki ya Kati, au migogoro inayovuruga usafirishaji wa bidhaa duniani. Kuzungumzia hili, hivi leo nimemualika Safari Fungo, mtaalamu wa masuala ya uchumi, utangamano wa…
Katika miaka ya hivi karibuni, sarafu za kidijitali maarufu kama cryptocurrency zimezidi kuvutia watu wengi duniani. Wapo waliopata faida kubwa, lakini pia wapo waliopoteza fedha nyingi kutokana na kushuka kwa thamani ya sarafu hizo. Leo katika Makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajiuliza: Je, sarafu za kidijitali ‘cryptocurrency’ ni uwekezaji wa kweli, au ni uwekezaji wenye hatari kubwa ambao watu…
Katika makala ya Gurudumu la Uchumi hivi leo, tunajadili nafasi ya kodi katika maendeleo ya uchumi, umuhimu wa kulipa kodi, na jinsi serikali na wananchi wanavyoweza kushirikiana kujenga uchumi imara na wenye manufaa kwa wote.
Msikilizaji nchi nyingi za Afrika Mashariki zimeendelea kukopa ili kufadhili maendeleo, na huku wadau wengine wakisema mikopo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi, Wengine wanaonya kuwa madeni yanapoongezeka kupita kiasi, serikali hulazimika kutumia fedha nyingi kulipa madeni hayo badala ya kuboresha huduma muhimu kama vile afya, elimu na ajira. Katika Makala ya Gurumu la Uchumi hivi leo, tunauliza: Je,…
Ufanyaji biashara na utumaji wa fedha kwa njia ya simu za kiganjani barani Afrika unakua kwa kasi, pochi za simu zimerekodi takriban asilimia 19 ya uingiaji wa pesa kwenye eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, huku wastani wa gharama ya utumaji pesa ukishuka hadi karibu asilimia 3.54 hii ni kwa mujibu wa benki ya dunia. Kwanye Makala ya Gurudumu la uchumi wiki hii, tunaangazia matumizi ya…
Msikilizaji Sekta ya maua nchini Kenya, ambayo kwa muda mrefu imekuwa miongoni mwa nguzo muhimu za uchumi na chanzo kikuu cha mapato ya fedha za kigeni, ikiingizia nchi zaidi ya dola bilioni moja za Marekani kila mwaka, sasa inakabiliwa na changamoto zinazotia wasiwasi kuhusu mustakabali wake.
Katika makala ya wiki hii, tunajadili ni kwanini nchi za Afrika zinapaswa kuongeza kasi ya ufanyaji wa biashara za wenyewe kwa wenyewe kukuza utangamano wa kikanda.
Tarehe 11 na 12 ya wiki ijayo, Jiji la Nairobi, Kenya litakuwa mwenyeji wa mkutano wa kwanza wa kihistoria wa ‘Africa Forward’ kati ya Ufaransa na Afrika, mkutano ambao unafanyika kwenye nchi inazungumza Kingereza, ambapo viongozi wa Afrika, wafanyabiashara na wabunifu vijana kutoka Afrika na Ufaransa watakongamana kwa siku mbili. Kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi hivi leo tunaangazia uhusiano…
Katika kipindi ambacho Afrika inaendelea kukabiliana na changamoto za kiuchumi na kijamii, teknolojia ya Akili Unde (AI) inaibuka kama nyenzo muhimu ya kuleta mabadiliko. Kutoka kilimo hadi afya, na kutoka elimu hadi utawala bora, ubunifu wa kidijitali unaanza kubadilisha namna matatizo ya muda mrefu yanavyotatuliwa.Katika makala hii, tunazungumza na Kevin Obote kijana mbunifu wa teknolojia ambaye…
Kupitia ripoti iliyozinduliwa juma hili na shirikisho la wazalishaji nchini Kenya, inaonyesha kuwa kusafirisha bidhaa katika njia muhimu za biashara za Afrika bado ni ghali na haitabiriki, ambapo wakati mwingine hugharimu hadi dola 7,000 za Marekani kwa kontena moja kati ya Nairobi na Lusaka. Kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, tumezungumza na Tobias Alando, mkurugenzi mtendaji wa…
Msikilizaji Katika miaka ya hivi karibuni, nchi nyingi za Afrika Mashariki zimekuwa zikifanya mageuzi makubwa ya kiuchumi. Mojawapo ya mageuzi hayo ni ubinafsishaji wa mashirika ya umma. Leo tunajiuliza, Je, ubinafsishaji ni kweli unasaidia uchumi kukua, au serikali inapaswa kubaki na umiliki wa mashirika muhimu?
Msikilizaji mara zote mgogoro wa mashariki ya kati, umekuwa na athari hasi za kiuchumi na biashara duniani, Swali kubwa tunajiuliza hivi leo ni Je, Afrika iko salama kiasi gani? Vita hivi vitaathiri vipi uchumi wa dunia — na gharama za maisha kwa mwananchi wa kawaida barani Afrika?
Benki ya Dunia inasema hata katika nchi zenye sheria za kisasa kuhusu usawa kazini, nchi hizo zimeshindwa kuzitekeleza, hadi sasa hakuna nchi iliyofikia kiwango cha juu cha usawa kazini, n ani asilimia kidogo tu ya wanawake wanaishi kwenye nchi zenye angalau sheria bora, huku mataifa 70 ikiwemo Misri, Madagascra na Somalia zikipiga hatua katika kuboresha mazingira ya usawa kati yam waka 2023 na…
Juma hili tunajadili kuhusu mustakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hasa wakati huu kukiwa na taarifa kuwa inakabiliwa na mgogoro wa kifedha. Taarifa zinaonesha kuwa Jumuiya hiyo inakabiliwa na upungufu wa bajeti unaofikia karibu dola za marekani milioni 89, pengo ambalo huenda likatatiza shughuli za Jumuiya hiyo, jambo ambalo limemfanya rais wa Kenya William Ruto ambaye ni mwenyekiti wa…
Mkutano wa siku tatu wa Serikali za Dunia mwaka 2026 huko Dubai umesisitiza kuhusu udhibiti wa Akili Mnemba, AI, mageuzi ya kidijitali, uchumi endelevu na thabiti duniani. Viongozi mbalimbali wametoa wito wa kuwepo ushirikiano thabiti wa kimataifa na mifumo mipya ya utawala inayoweza kutazamia changamoto za siku zijazo lakini pia kushughulikia masuala ya pamoja kama vile mabadiliko ya hali ya…
Msikilizaji mataifa makubwa kama Marekani, China, Urusi na Ulaya yanaendelea kushindana kiuchumi, kuanzia kwenye biashara, teknolojia, nishati na rasilimali. Lakini je, ushindani wao unaathiri vipi uchumi wa dunia? Leo kwenye Makala ya Gurudumu la Uchumi tunajadili, “Athari za Kiuchumi kwa Dunia Zitokanazo na Ushindani wa Maslahi ya Kiuchumi kati ya Mataifa Makubwa.”
Msikilizaji Rais wa Kenya, William Ruto, ameendelea kusisitiza azma ya kuifanya nchi yake kuwa Singapore ya Afrika, suala ambalo limeibua mjadala mkali nchini humo baadhi wakisema ni suala ambalo halitawezekana chini ya utawala wake na wengine wakiona ni jambo linalowezekana. Kwenye makala yetu leo tunajiuliza, je, Kenya inaelekea huko? Ndoto hii inawezekana au ni siasa?
Msikilizaji jamii ya Wamaasai kwa muda mrefu imekuwa ikitegemea ufugaji wa mifugo kama chanzo kikuu cha riziki na chakula, hata hivyo, mabadiliko ya tabianchi yaliyoambatana na ukame wa mara kwa mara yamilazimisha jamii hii kutafuta mbinu mbadala za kujipatia kipato, mojawapo ni ufugaji wa samaki.